NI Russia v Portugal, Spain v France, Poland v England!!
Zipo
Mechi KIBAO Ijumaa na Jumanne ijayo, Mechi za Mchujo kwa Kanda ya Ulaya
kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil,
lakini ni Mechi 3 ambazo ndizo zimejitokeza kuwa ndizo za mvuto na,
pengine, zitakuwa tamu.Russia VS Portugal
Mechi hii itachezwa Ijumaa Oktoba 12 kuanzia Saa 12 Jioni saa za Bongo na ni Mechi ya Kundi F inayozikutanisha Timu ambazo zimeshinda Mechi zao zote mbili za kwanza.
MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 2]
KUNDI F
1 Russia Pointi 6
2 Portugal 6
3 Luxembourg 1
4 Northern Ireland 1
5 Azerbaijan 1
6 Israel 1
Baada ya kutofanya vyema kwenye EURO
2012, Russia ikambadili Kocha Guus Hiddink na kumweka aliekuwa Kocha wa
England, Fabio Capello, ambae katika Mechi ya mwisho aliingoza Russia
kuinyuka Israel 4-0 ugenini.
Portugal, chini ya Kocha Paulo Bento, ni
Timu imara na yenye mvuto huku kilingeni ikiongozwa na Supastaa
Cristiano Ronaldo ambae, pengine, huenda akaikosa Mechi hii baada ya
Jumapili iliyopita kujiumiza bega wakati Klabu yake Real Madrid
ilipotoka 2-2 na Barcelona.
Spain vs France
Ndani ya Uwanja wa Vicente Calderon
Jijini Madrid, Mabingwa wa Ulaya na Dunia, Spain, watawakaribisha France
katika Mechi ya Kundi I ambalo Mabingwa hao wamecheza Mechi moja tu
walipowafunga Georgia bao 1-0 kwa bao la lala salama la Roberto Soldado.
MSIMAMO
KUNDI I
1 France Mechi 2 Pointi 6
2 Spain Mechi 1 Pointi 3
3 Georgia Mechi 2 Pointi 3
4 Finland Mechi 1 Pointi 0
5 Belarus Mechi 2 Pointi 0
France, chini ya Kocha wao Didier
Deschamps, wapo juu kwenye Kundi hili baada ya kushinda Mechi zao zote
mbili za kwanza dhidi ya Finland na Belarus.
Mara ya mwisho Timu hizi kukutana
ilikuwa kwenye EURO 2012 kwenye Robo Fainali na France kuendeshwa
mchakamchaka na kunyukwa bao 2-0 kwa bao za Xabi Alonso.
Poland vs England
Kundi H, baada ya Mechi mbili mbili,
England, Poland na Montenegro wote wana Pointi 4 kila mmoja baada ya
kila mmoja kushinda Mechi moja na sare moja na hili kuifanya Mechi
itakayochezwa huko Poland kuwa ni muhimu mno katika Kundi hili.
VIKOSI VINATEGEMEWA KUWA HIVI:
England:Hart,Johnson, Cahill, Lescott, Baines,Lampard, Gerrard,Milner, Cleverley, Oxlade-Chamberlain,Defoe Ukraine:Pyatov,Husyev, Mikhalik, Khacheridi, Selin,Tymoshchuk,Yarmolenko, Garmash, Konoplyanka,Devic, Zozulya
MSIMAMO:
KUNDI H
1 Montenegro Mechi 2 Pointi 4
2 England Mechi 2 Pointi 4
3 Poland Mechi 2 Pointi 4
4 Ukraine Mechi 1 Pointi 1
5 San Marino Mechi 1 Pointi 0
6 Moldova Mechi 2 Pointi 0
Kwa Poland, Straika Robert Lewandowski, anaechezea Klabu ya Germany Borussia Dortmund, ndie ufunguo wa mafanikio yao.
England, safari hii, itaingia bila
mkongwe wao John Terry alietangaza kustaafu baada ya kuandamwa kwa
kashfa ya ubaguzi na kuadhibiwa kwa hilo na pia huenda itamkosa mkongwe
mwengine mwenzake Terry huko Chelsea, Frank Lampard, ambae ana maumivu.
RATIBA MECHI ZOTE
ULAYA-Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014
[Saa za Bongo]
Ijumaa Oktoba 12
18:00 Russia v Portugal
18:30 Finland v Georgia
19:00 Armenia v Italy
19:00 Faroe Islands v Sweden
19:00 Kazakhstan v Austria
20:00 Albania v Iceland
20:00 Czech Republic v Malta
20:30 Liechtenstein v Lithuania
20:30 Turkey v Romania
21:00 Belarus v Spain
21:00 Bulgaria v Denmark
21:00 Moldova v Ukraine
21:15 Slovakia v Latvia
21:30 Estonia v Hungary
21:30 Netherlands v Andorra
21:30 Serbia v Belgium
21:45 Greece v Bosnia-Hercegovina
21:45 Rep of Ireland v Germany
21:45 Wales v Scotland
22:00 England v San Marino
22:00 Luxembourg v Israel
22:30 Macedonia v Croatia
22:30 Switzerland v Norway
22:45 Slovenia v Cyprus
Jumanne Oktoba 16
Albania v Slovenia
Andorra v Estonia
Belarus v Georgia
Belgium v Scotland
Bosnia-Hercegovina v Lithuania
Czech Republic v Bulgaria
Hungary v Turkey
Iceland v Switzerland
Israel v Luxembourg
Latvia v Liechtenstein
Macedonia v Serbia
Portugal v Northern Ireland
Romania v Netherlands
Russia v Azerbaijan
San Marino v Moldova
Slovakia v Greece
Spain v France
Ukraine v Montenegro
2000 Cyprus v Norway
2100 Faroe Islands v Rep of Ireland
2130 Austria v Kazakhstan
2130 Croatia v Wales
2145 Germany v Sweden
2145 Italy v Denmark
2200 Poland v England
FAHAMU:
-ULAYA yapo Makundi 9
***Washindi 9 wa kila Kundi
wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi
nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano
kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo,
zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia
Fainali.***
Brazil 2014 FIFA World Cup Stadiums
2014 World Cup in Brazil StadiumManaus Proposed 2014 FIFA World Cup Stadium
Natal Proposed 2014 FIFA World Cup Stadium
Brasília Proposed 2014 FIFA World Cup Stadium
Natal Proposed 2014 FIFA World Cup Stadium
Brasília Proposed 2014 FIFA World Cup Stadium
No comments:
Post a Comment