MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Bolton Wanderers, Fabrice Muamba ambaye alikumbwa na tatizo la moyo wake kusimama wakati wa mchezo baina ya timu yake na Totenham Hotspurs
Machi mwaka huu amerejea kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa White Hart Lane mahali ambao ndipo alipoanguka. Muamba ambaye moyo wake ulisimama kwa dakika 78 baada ya kuanguka wakati wa mchezo huo wa Kombe la FA baadae alipona kabisa kutokana na tatizo hilo lakini alilazimika kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 24 kutokana na ushauri wa madaktari.
Akitembea uwanjani wakati wa kipindi cha mapumziko katika mchezo wa Europa League kati ya Spurs na Maribor ya Slovenia, Muamba alionyesha mahali ambapo alianguka na baade kuzungumza na mashabiki waliokuwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo.
Muamba aliwashukuru mashabiki wa Spurs ambao walikuwepo na kumuombea wakati alipopata tatizo hilo na kusema kwamba hatawasahau kamwe katika maisha yake.
Timu ya madaktari wa Spurs na Bolton walijaribu kuokoa maisha ya Muamba kwa muda wa dakika 20 baada ya kuanguka kabla ya kuondolewa na ukimbizwa hospitali ambapo alilazwa kwa kipindi cha wiki nne.Machi mwaka huu amerejea kwa mara ya kwanza katika Uwanja
wa White Hart Lane mahali ambao ndipo alipoanguka. Muamba ambaye moyo
wake ulisimama kwa dakika 78 baada ya kuanguka wakati wa mchezo huo wa
Kombe la FA baadae alipona kabisa kutokana na tatizo hilo lakini
alilazimika kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 24 kutokana na ushauri
wa madaktari.
Muamba
_________________________________________
INTER, PARTIZAN, LYON, LEVERKUSEN, KAZAN, METALIST NA HANOVER 96 ZATINGA 32 BORA EUROPA LEAGUE.
MABAO mawili yaliyofungwa na Rodrigo Palacio yaliiiwezesha Inter Milan kutinga katika hatua ya mtoano wa Europa League wakati Atletico Madrid walijikuta wakifungwa kwa mara ya kwanza katika mechi 16 walizocheza nchini Ureno. Milan ambao waliwafunga Partizan Belgrade ya Serbia kwa mabao 3-1
wameungana na timu za Bayer Leverkusen, Rubin Kazan, Metalist Kharkiv, Hanover 96 na Olympique Lyon katika hatua hiyo ya mtoano ambayo itashirikisha timu 32.
Rubin Kazan ya Urusi ilifanikiwa kuongoza katika kundi H wakiwa na alama 10 sawa na Inter baada ya kuifunga Neftchi Baku ya Azerbaijan kwa bao 1-0 wakati Leverkusen na Metalist nazo pia zikikabana koo kwa alama 10 katika kundi K baada ya kushinda michezo yao ya jana usiku. Lyon waliendeleza rekodi yao nzuri kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mshindi wa pili wa michuano hiyo msimu uliopita Athletic Bilbaona kushika usukani wa kundi I wakifuatiwa na Sparta Prague katika nafasi ya pili.
Hugo Lloris (Olympique Lyonnais)Goalkeeper Hugo Lloris of Olympique Lyonnais celebrates his team's second goal during their UEFA Europa League matchday four game against Athletic Club
No comments:
Post a Comment