BUKOBA SPORTS

Thursday, December 6, 2012

CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP: NI UGANDA vs KENYA - FAINALI

MATOKEO
Kenya  2 (Baraza 30’, 80’) Zanzibar  2 (Khamis 20’ Morris 75’) (Kenya wins on penalties)
Uganda 3 (Okwi 12’, Ssentongo 53’, 73’) Tanzania   0

TIMU ya Taifa ya Zanzibar, leo imeondolewa katika michuano ya CECAFA Tusker Chalenji baada ya kufungwa na timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars. Zanzibar Heroes imeondolewa katika mashindano hayo kwa njia ya penati baada ya dakika 120 kumalizika kila timu ikiwa na mabao 2-2.
Baada ya muda huo kumalizika huku timu zote zikitoka sare 2-2, ndipo iliamuliwa zipigwe penati ambapo Kenya ilishinda kwa penati 4 huku wenzao wa Zanzibar wakiambulia penati 2. Harambee Stars sasa itacheza  mshindi wa mechi ya pili  iliyomalizika muda si mrefu  Uganda ambayo imeweza kuwafunga Kilimanjaro Stars goli 3 -0. mpira ambao ulikuwa nivute nikuvute na kupaniana sana. Kipindi cha pili mwishoni kumetokea kukatika kwa umeme refa akasimamisha mtanange huo kwa muda na kisha umeme ukarudi na kumalizia mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment