BUKOBA SPORTS

Saturday, January 26, 2013

AFCON 2013: NIGERIA 1 vs ZAMBIA 1

Mechi kati ya miamba wawili wa soka barani Afrika Nigeria na Zambia imemalizika huku timu hizo zikitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.
Mechi hiyo ambayo ilikisiwa kuwa moja ya mechi ngumu zaidi katika hatua ya makundi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini.
Mechi hizo ilianza kwa mashambukizi katika pande zote na kunako dakika ya 25,mlinda lango wa Zambia Davies Nkausu alimfanyia madhambi mshambulizi wa Nigeria Ahmed Musa na hivyo refa wa mechi hiyo kutoa penalti kwa Nigeria.

Mchezaji wa Zambia wakati wa mechi yao na Ethipia
Lakini mcheza kiungo wake ambaye pia anaichezea klabu ya Chelsea akapoteza penalti hiyo na hivyo kuwapa mabingwa hao watetezi nafasi nyingine ya kupumua.
Katika kipindi hicho cha kwanza timu hizo mbili zilionekana kutoshana nguvu huku pande zote zikifanya mashambulio ya mara kwa mara.

Kufikia wakati wa mapunziko, hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwezio.
Nigeria ilianza kipindi cha pili kwa kasi zaidi na kufanya mashambulio kadhaa katika lango la Chipolopolo.
Na baada ya kupoteza mkwaju wa penalti John Obi Mikel, alijiimarisha zaidi kipindi cha pili na kunako dakika ya 56 Nigeria ikapata bao lake la kwanza kupitia kwa mshambulizi wake matata Emmanuel Emenike.
Bao hilo lilionekana kuwachanganya wachezaji wa Zambia na kuwapa wasi wasi hatua iliyomlazimisha kocha wake kufanya mabadiliko.
Mulenga Mukuka aliondolewa na mahala pake kuchukuliwa na Chisamba Lungu, naye Collins Mbesuma akaingia kuchukua mahala pa nahodha wa Chipolopolo Christopher Katongo.
Mabadiliko hayo yaliipa nguvu zaidi Zambia na kunako dakika ya 72, nusura Zambia isawazishe kupitia kwa mchezaji huyo wa ziada Mukuka.
Kunako dakika ya 84 mlinda lango wa Nigeria alimuangusha mshambuliaji wa Zambia Emmanuel Mayuko, na refa wa mechi hiyo sawa na alivyokuwa amefanya katika kipindi cha kwanza akaipa Zambia penalti ambayo iliwekwa kimyani na kipa za Chipolopolo Kennedy Mweene.
Nigeria sasa ina alama mbili sawa na Nigeria na itabidi washinde mechi zao za mwisho siku ya jumapili ili kufuzuz kwa hatua ra robo fainal.
Awali Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, amewaandikia wachezaji wa Super Eagles na kuwapa ushauri wa jinsi ya kucheza mechi hiyo.
Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi, vile vile alifika mbele ya viongozi wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, kuelezea kwa nini hawakushinda mechi yao ya ufunguzi.
Mechi ya pili katika kundi hilo kati ya Ethiopia na Burkina Faso kuanza mwendo wa saa tatu za usiku majira ya Afrika mashariki.Mashabiki wa timu ya Nigeria
 
Zambia 1 Nigeria 1 - African Nations Cup Group C 
UWANJA: Mbombela Stadium
WAFUNGAJI
Zambia - Kennedy Mweene 85 penalty
Nigeria - Emmanuel Emenike 57
Missed penalty: John Obi Mikel 26

Halftime: 0-0
VIKOSI:
Zambia: 16-Kennedy Mweene; 6-Davies Nkausu, 18-Emmanuel
Mbola, 13-Stopilla Sunzu, 4-Joseph Musonda; 3-Chisamba Lungu
(23-Mukuka Mulenga 66), 8-Isaac Chansa (21-Jonas Sakuwaha 73),19-Nathan Sinkala, 17-Rainford Kalaba, 11-Chris Katongo
(9-Collins Mbesuma 66); 20-Emmanuel Mayuka

Nigeria: 1-Vincent Enyeama; 3-Elderson Echiejile, 22-Kenneth
Omeruo, 14-Godfrey Oboabona, 17-Ogenyi Onanzi; 13-Fegor Ogude,10-John Obi Mikel, 20-Nosa Igiebor (4-Obiora Nwankwo), 11-Victor Moses (8-Brown Ideye 79); 9-Emmanuel Emenike 7-Ahmed Musa (15-Ikechukwu Uche 89)
Referee: Grisha Ghead (Egypt)

No comments:

Post a Comment