KUBAKI CRYSTAL PALACE HADI JULAI!
Wilfried Zaha amefaulu upimaji afya yake
Klabuni Manchester United na kusaini Mkataba wa Miaka 5 na Nusu na
hivyo kukamilisha Uhamisho wa Pauni Milioni 15 kutoka Crystal Palace.
Zaha, mwenye Miaka 20 ambae ni mzaliwa
wa Ivory Coast, Msimu huu atamalizia akiwa Crystal Palace ili kuisaidia
Klabu hiyo kufuzu kupanda Daraja na kuingia Ligi Kuu England.
Man United italipa Pauni Milioni 10
mbele na Dau hilo linaweza kupanda na kufikia Pauni Milioni 15
ikitegemea Mechi ambazo Zaha atacheza na mafanikio yake wakati akiwa Old
Trafford.
Zaha, ambae alijunga na Crystal Palace
akiwa na Miaka 12 tu baada ya Familia yake kuhamia Uingereza yeye akiwa
na Miaka minne, anatarajiwa kuitwa kwenye Kikosi cha England
kitakachocheza na Brazil hapo Februari 6 Uwanjani Wembley.
Msimu uliopita, Zaha ndie alietwaa Tuzo ya kuwa Mchezaji mdogo Bora kwenye Ligi England.
WASIFU WA WILFRIED ZAHA
>KUZALIWA: 10 Novemba 1992 huko Ivory Coast na kuhamia England akiwa na Miaka minne
>POZISHENI: Winga au Straika
>KLABU: Crystal Palace (2009-hadi sasa)
>KUANZA KUCHEZA: Crystal Palace v Cardiff (27 Machi 2010)
>MECHI: 124
>MAGOLI: 15
>TIMU ya TAIFA ENGLAND U-19: Mechi 2
>TIMU ya TAIFA ENGLAND U-19:: Mechi 5
>TIMU ya TAIFA ENGLAND: Mechi 1
No comments:
Post a Comment