Timu za kundi C leo ziko kibaruani kusaka pointi tatu muhimu kutafuta nafasi ya kucheza robo fainali.
Vinara wa kundi hilo Burkina Faso yenye pointi 4 itakuwa ikihangaishana na mabingwa watetezi Zambia yenye pointi 2.
Timu nyingine za kundi hilo ni Ethiopia yenye pointi 1 itakayomenyana na Nigeria yenye pointi 2.
Kikosi cha Nigeria
Mechi hizo zitachezwa kwa wakati mmoja.
Burkina Faso kwa mara ya kwanza ilicheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1978, wakati huo ikijulikana kama Upper Volta. Na walitolewa katika hatua za mwanzo tu za michuano hiyo.
Ilipita miaka 18, timu hiyo iliposhiriki kwa mara ya pili mwaka 1996, wakati mashindano hayo yalipoandaliwa nchini Afrika Kusini. Pia wakati huo walitolewa katika hatua ya makundi. Miaka miwili baadaye walipoandaa michuano hiyo ilimaliza katika nafasi ya nne, yakiwa ni mafanikio makubwa zaidi kufikiwa na timu hiyo. Wachezaji wengi wa Burkina Faso wanacheza nje ya nchi, hususan Ufaransa.

Nao mabingwa watetezi Zambia itabidi wakaze musuli, kwani wakishindwa katika mchezo wake na Burkina Faso tayari watakuwa wamepoteza kombe wanaloshikilia.
Group C Consists Of
No comments:
Post a Comment