Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika,
Chipolopolo ya Zambia, leo wamebanduliwa nje ya mashindano hayo baada
ya kutoka sare 0-0 na Burkina Faso katika mechi yao ya mwisho ya
makundi.
Burkina
Faso ilianza mechi hiyo kwa bahati mbaya baada ya nyota wake Alain
Traore kupata jeraha na kuondolewa uwanjani baada ya dakika kumi pekee.
Traore amefunga magoli matatu zikiwemo mbili wakati wa mechi yao dhidi ya Ethiopia ambayo walishinda kwa magoli manne ya yai.
Dakika chache baadaye Davis Nkausu, wa Zambia
vile vile alijeruhiwa na kuondolewa uwanjani na mahala pake kuchukuliwa
na Joseph Musonda baadda ya kugongana na mlinda lango wa Burkina Faso.
Kufikia wakati wa mapunziko timu hizo mbili zilikuwa zimetoshana nguvu ya kutofangana bao lolote.
Katika kipindi cha pili Zambia ilifanya mashambulio kadhaa katika lango la Burkina Faso, lakini juhudi zao zligonga mwamba.
Mechi hiyo ilimalizika huku timu hizo mbili
zikigawamna alama moja kila moja na hivyo Burkina Faso kusonga mbele
baada ya kukusanya jumla ya alama tano nayo zambia ikiridhika la alama
mbili.
Nigeria imeongoza kundi hilo kwa jumla ya alama tano huku Ethiopia ikivuta mkia na alama moja.
Kabla ya mechi hiyo Zambia ilikuwa na alama
mbili na ilihitaji ushindi katika mechi ya leo ili ifuzu kwa raundi
iajyo sawa na Nigeria.
Hata hivyo mabingwa hao watetezi watajialaumu baada ya kukoso nafasi nyingi za kufunga wakati wa mechi hiyo.
Collins Mbesuma na Rainford Kalaba hawakuonyesha
mchezo mzuri kama iliyotarajiwa na uamuzi wa kocha mkuu wa kumuacha nje
nahodha wa Chipolopolo huenda ukashutumiwa vikali, na mashabiki wa
Zambia.
No comments:
Post a Comment