BUKOBA SPORTS

Friday, January 25, 2013

AUSTRALIA OPEN: ANDY MURRAY USO KWA USO NA NOVAK DJOKOVIC KWENYE FAINALI.

MCHEZAJI tenisi nyota kutoka Uingereza, Andy Murray amefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya wazi ya Australia baada ya kumfunga Roger Federer wa Switzerland katika mchezo nusu fainali uliofanyika katika Uwanja wa Rod Laver Arena jijini Melbourne. Murray anayeshika namba tatu katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanaume alifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kumfunga Federer anayeshika namba mbili kwa ubora kwa 6-4 6-7 6-3 6-7 6-2.Sasa Murray atakwaana na Novak Djokovic anayeshika namba moja katika orodha hizo katika mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Jumapili. Kwa upande wanawake wanadada nyotakutoka Italia Sara Errani na Roberta Vinci wa Italia wamefanikiwa kushinda taji la michuano hiyo la wawili wawili baada yakuwafunga Ashleigh Barty na Casey Dellacqua kwa 6-2 3-6 6-2. Errani na Vinci walizima ndoto za Barty na Dellacqua ambao ni raia wa Australia kunyakuwa taji hilo kwa mara ya kwanza kwenye ardhi ya nyumbani kwao.

Andy MurrayScotland's finest: Murray was roared on by his fans Murray was roared on by his fans
Favourite: Defending champion Djokovic beat Murray in the 2011 final
Defending champion Djokovic beat Murray in the 2011 final

No comments:

Post a Comment