Leroy Fer
Everton imekubali kulipa kitita cha puani milioni saba kumsajili mcheza kiungo wa FC Twente, kutoka Uholanzi Leroy Fer.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amefunga
magoli kumi baada ya kucheza mechi ishirini na tisa kwa klabu hiyo ya FC
Twente chini ya Kocha Steve McClaren.Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwa wavotu wa klabu hiyo, mchezaji huyo sasa anatarajiwa kufika England kujadiliana kuhusu mshahara wake na pia kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Everton, ambayo inacheza na West Brom siku ya Jumatano inashikilia nafasi ya tano kwenye msururu wa ligi kuju ya Premier, alama tatu nyumba ya Tottenham.
Fer, ameichezea timu ya taifa ya Uholanzi mechi mbili na anajulikana kwa jina la utani "The Bouncer"kutokana na umbo lake.
Wakiwa kwenye ndege Leroy Fer (kushoto), na agent Rob Jansen na girlfriend Xenia (kulia)
No comments:
Post a Comment