BUKOBA SPORTS

Sunday, January 27, 2013

FA CUP: MANCHESTER CITY 1 vs STOKE CITY 0, PABLO ZABALETA AISAIDIA CITY KUFUZU RAUNDI YA 5 YA FA.

Pablo Zabaleta amefunga bao kunako dakika za mwisho mwisho na kuisaidia Manchester City kuipiku Stoke City kwa bao moja kwa bila na kufuzu kwa raundi ya tano ya michuano ya kuwania kombe la FA.
Manchester City haikutumia nafasi walizopata kufunga wakati wa mechi hiyo.
Juhudi za washambuliaji wake David Silva na Carloz Tevez hazikufua dafu pale mikwaju yao ilipogonga mlingoti.
Kipa wa Stoke Thomas Sorenson vile vile alifanya kazi ya ziada kuokoa mikwaju ya washambuliaji hao wa Manchester City.

Stoke haikufanya mashambulizi yoyote ya maana wakati wa mechi hiyo.

Lakini wakati mechi hiyo ilipoonekana kuisha kwa timu hizo mbili kutoshana nguvu, Sergio Aguero alimpa pasi nzuri Zabaleta ambaye aliiweka kimyani na kuwaacha mashabiki wa Stoke vinywa wazi.

Mchezaji wa ziada ya Stoke Cameron Jerome, alipata nafasi nzuri sana ya kusawazisha lakini, akaupiga mpira ovyo licha ya kuwa katika nafasi nzuri na kipa pekee.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Manchester City katika uwanja huo wa Stoke tangu mwaka wa 1999, wakati timu hizo mbili zilikuwa
zinacheza ligi daraja ya pili.David Silva wa City akikwatuliwa na mchezaji wa Stoke City defender Ryan Shawcross

Javi Garcia akimwangalia refa Howard Webb baada ya ndivyo sivyo ya Glenn Whelan na kutopewa kwake kadi yoyote Aleksandar Kolarov wa City akionesha kuumia baada ya kosa kosa
Michael Kightly na Carlos Tevez wakichuana FA Cup
Silva akichuana na mchezaji wa Stoke

VIKOSI:
Stoke City: Sorensen, Shotton, Huth, Shawcross, Wilkinson (Whitehead 72), Kightly (Jerome 66), Nzonzi, Whelan, Etherington, Walters, Jones (Crouch 72)
Subs not used: Nash, Owen, Adam, Upson
Booked: Shotton
Manchester City: Pantilimon, Zabaleta, Kompany (Clichy 39), Lescott, Kolarov (Aguero 62), Garcia, Barry, Milner, Tevez (Rodwell 85), Silva, Dzeko
Subs not used: Hart, Sinclair, Rekik, Lopes
Goal: Zabaleta 85
Booked: Kolarov, Milner
Referee: Howard Webb 


RATIBA LEO FA CUP
RAUNDI YA 4

Jumapili Januari 27

[SAA 9 Mchana]

Brentford v Chelsea

[SAA 11 Jioni]

Leeds United v Tottenham Hotspur

[SAA 1 Usiku]

Oldham Athletic v Liverpool

No comments:

Post a Comment