BUKOBA SPORTS

Thursday, January 31, 2013

KIPA BURLAND AWACHOMOLEA NJE THE BLUES "CHELSEA"


Kipa wa Birmingham Jack Butland
Jack Butland amekataa fursa ya kujadiliana na Chelsea kuhusu mshahara wake na masharti ya utendaji kazi baada ya klabu yake kuafiki ombli la Chelsea la kumsajili kipa huyo wa Uingereza kwa kitita cha pauni milioni tatu na nusu.
Wiki iliyopita Birmingham City, ilikiri ipo tayari kwa mazungumzo na klabu yoyote inayotaka kusajili mchezaji yeyote kutokana na matatizo ya kifedha.
Lakini, Butland, 19, amekataa fursa hiyo ya kufanya mazungumzo na Chelsea, akisema nia yake kuu ni kutaka kucheza mara kwa mara na haoni kuwa Chelsea, itampa nafasi hiyo.

Butland, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza Uingereza, mwezi Agosti, mwaka uliopita wakati wa mechi yao dhidi ya Italia ambayo walishinda kwa mabao mawili kwa moja, anataka kusalia na Birmingham City hadi mwisho wa msimu huu.
Mwezi uliopita, kaimu mwenyekiti wa klabu hiyo Peter Pannu, alisema kuwa Birmingham City, huenda ikalazimika kumuuza mchezaji huyo mwezi huu.
Vilabu vya Southampton na Everton, vilijaribu kumsajili mchezaji huyo msimu uliopita na pia amehusishwa na vilabu vya Liverpool, Fulham, Newcastle na Manchester City.
Mmiliki wa Birmingham City Carson yeung

No comments:

Post a Comment