MAANDALIZI YA MAPAMBANO YA NGUMI JUMAMOSI HII YAKUIANDAA TIMU YA MKOA WA KAGERA KWA AJILI YA MASHINDANO YA LIGI YA TAIFA YA NGUMI DAR ES SALAAM.
Mwalimu akiangalia wanafunzi wake wakijifua leo hii kwenye fukwe za Kiroyera Nyoosha viungo.. mazoezi yakiendelea.. Willy akiendelea kuongea na vijana Ufukeni hapo kuhusu mitanange hiyo ya Jumamosi Mwalimu mfano wa kuigwa.. Bw. Willy O.Rutta ambaye ni katibu wa chama cha ngumi mkoa wa Kagera akiteta na wanamasumbwi waliojitokeza leo hii. Akiongea na Bukobasports.com Willy amesema kuwa itakuwa ni siku ya kipekee siku hiyo ya jumamosi na pia wasanii kutoka Dar es salaam watakuwepo kwa Burudani na Wanamasumbwi Maarufu watakuwepo siku hiyo. Mwanamasumbwi(kushoto) akiwa amechemka kweli kweli na mazoezi leo asubuhi Zoezi likiendelea .. mwalimu na yeye akifanya mazoezi hapa(kulia) ni Bw. Willy katibu wa chama cha ngumi mkoa wa Kagera akionesha kipaji hapa. Katibu wa chama cha ngumi mkoa wa Kagera Bw. Willy O.Rutta akiongea kuhusu mapambano hayo ya jumamosi yatakayofanyika kwenye ukumbi wa Lina's Bukoba Wakiruka kamba
No comments:
Post a Comment