BUKOBA SPORTS

Wednesday, January 23, 2013

PUYOL AJIFUNGA NA BARCELONA HADI 2016


Carles Puyol akishikana mkono na Sandro Rosell baada ya kumwaga wino.
President, Sandro Rosell, Vice-president, Josep María Bartomeu and Director of Football, Andoni Zubizarreta were with the player at the contract signing.


NAHODHA wa Barcelona, Carles Puyol amesaini mkataba mpya utakaomweka hadi mwaka 2016.

Puyol alimwaga wino katika hafla iliyofanyika juzi.

Alisema: "Mtazamo wangu ilikuwa ni kuendelea kucheza hapa, nataka kubaki hapa kwa miaka mingi iwezekanavyo. Nashukuru kwa juhudi zilizofanywa na klabu, kusaini mkataba huu ni muhimu sana, lakini lililo muhimu zaidi ni kuumaliza."

Puyol pia alizungumzia muda wake mrefu kwenye soka:
"Kubaki fiti ni jambo muhimu sana nafahamu kwamba natakiwa kujilinda ndani na nje ya uwanja. Hicho ndicho nitakachojaribu kukifanya.

"Natakiwa kulifanya hili msimu mmoja hadi mwingine, lakini matumaini yangu ni kuendelea kucheza soka hadi nikiwa na miaka 40."

Carles Puyol

No comments:

Post a Comment