Straika huyo hatari ambaye ameifungia Man United Mabao 22 katika Mechi 28 huku Bao 18 zikiwa kwenye Ligi Kuu England alihamia Old Trafford mwanzoni mwa Msimu huu.
Van Persie, akifurahia mwanzo mzuri na
Man United, ametamka: “Arsenal ni Klabu kubwa na Siku zote nilijisikia
vizuri kuwa nao lakini baada ya Miaka 8 nilijisikia nitafute changamoto
nyingine. Changamoto hii nimeipata Manchester United. Nimezungukwa na
Mabingwa.”
Aliongeza: “Nahisi huu ni wakati muafaka
kuhamia hapa. Kila Siku inaniambia nilifanya uamuzi sahihi. Sidhani
ingekuwa safi kuja mapema. Nimekuja hapa kupata changamoto kubwa. Hakuna
kitu kibaya kuhusu Arsenal. Hakuna Mchezaji mkubwa kuliko Klabu,
Arsenal Siku zote itakuwepo kugombea Makombe na kuwa juu. Lakini baada
ya Miaka 8 nilikuwa tayari kuondoka na kujaribu kitu kipya.”

Akizungumzia kuhusu hali yake tangu atue
Old Trafford, Robin van Persie amesema kila Mtu amekuwa mwema kwake na
imemsaidia sana kujisikia nyumbani.
Amesema: “Nasikia furaha. Naona vitu
ambavyo sijaviona muda mrefu. Nilipotua Arsenal kwa mara ya kwanza
niliona vitu toka kwa Dennis Bergkamp na Thierry Henry ambavyo nilikuwa
sijaviona maishani. Sasa naviona vitu hivyo tena na hilo linanifanya
niwe na furaha.”
No comments:
Post a Comment