Burkina Faso, imetinga fainali baada ya kuilaza Ghana kwa njia ya mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika dakika 120 za mchezo, ukiwa ni mchezo wa pili wa nusu fainali za kombe la mataifa ya Afrika.
Ghana ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa
kucheza fainali, walishindwa kutamba mbele ya vijana wa Burkina Faso na
kulazimika mikwaju ya penalti inatumika.
Ghana walipata penalti mbili tu, huku mbili zikipigwa nje na moja ikipanguliwa na mlinda mlango wa Burkina Faso.
Sasa Ghana itachuana na Mali kumtafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi.
Jumapili, ndiyo siku yenyewe ya kujulikana bingwa. Je, ni Nigeria au Burkina Faso? Dakika 90 zitatoa jibu la kitendawili hicho.
Nenda ukatupaishe Fainali ndugu yangu .... nenda... Burkina Faso wakishangilia baada ya penati ya goli la ushindi kutupiwa nyavuniWachezaji wa Burkina Faso wakimkumbatia kipa wao
Mchezaji wa Burkina Faso Aristide Bance kulia akiziona nyavu za Ghana
Mchezaji wa Ghana Mubarak Wakaso akitupia kwenye kipindi cha kwanza.
Mchezaji wa Burkina Faso Jonathan Pitroipa akishangazwa na upewaji wa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu, kikubwa ni kujitupa eneo hatari la penati
We toka tu ...
Kwenye mikwaju ya Penati na hapa ni kikosi cha Ghana
Mashabiki wa Ghana wakishangilia
Usipime....
No comments:
Post a Comment