BUKOBA SPORTS

Wednesday, February 6, 2013

AFCON 2013: MALI 1 vs NIGERIA 4, ELDERSON ECHIEJILE AISOGEZA NIGERIA FAINALI!!


Nigeria imetinga fainali baada ya kuicharaza Mali magoli 4-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Afrika.
Elderson Echiejile aliifungia magoli mawili ya kwanza katika dakika ya 25 na 30 ya mchezo.
Goli la tatu lilifungwa na Emenike katika dakika ya 44 baada ya mpira aliopiga kumgonga Momo Sissoko wa Mali.
Hadi mapumziko Nigeria ilikuwa ikiongoza kwa 3-0.
Ahmed Musa alizidi kuleta majonzi kwa mashabiki wa Mali alipofunga bao la nne katika 60.
Mali ilizidi kusaka bao, katika dakika ya 70 Cheikh Diarra aliifungia timu yake bao la kufutia machozi.
Nigeria kuingia nusu fainali waliwabwaga Ivory Coast 2-1, timu ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kucheza fainali kutokana na ubora wa wachezaji wake.
Nayo Mali iliwatoa wenyeji wa mashindano Afrika Kusini kwa njia ya mikwaju ya penalti 3-1 baada ya timu hizo kucheza dakika 120 zikiwa zimefungana goli 1-1.
Timu nyingine katika nusu fainali za Afcon ni Ghana itakayokwaruzana na Burkina Faso. Ghana waliitoa Cape Verde katika hatua ya robo fainali kwa magoli 2-0, huku Burkina Faso wakiifunga Togo kwa goli 1-0.
Sasa Nigeria inamsubiri mshindi kati ya Ghana na Burkina Faso zinazocheza mchezo wa pili wa nusu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.
Nigeria's Brown Ideye slides into score and help send his team into the final
Mshambuliaji wa Nigeria Brown Ideye akifanya juhudi ili timu yake kuibuka na ushindi
Reflection: Mali's participation in the competition isn't over and they will play the losers of tonight's game in the third place play-off
Hoi.... Mali sasa kupigania nafasi ya Tatu
Party atmosphere: Nigerian fans celebrate their progress
Mashabiki wa Nigerianwakishangilia baada ya timu yao kushinda goli 4-1 dhidi ya Mali

No comments:

Post a Comment