Kipa wa 'Indomitable Lions'ya Cameroon, Effala Komguep akiokoa hatari langoni mwake wakati wa mechi yao dhidi ya Taifa Stars ya Stars ya Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Stars ilishinda 1-0.
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo imeshinda Bao 1-0 dhidi ya Cameroon, Timu ambayo ipo nafasi 57 juu yake kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani, katika Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa iliyochezwa Siku ya Kalenda ya FIFA, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaama.
Bao la ushindi kwa Tanzania lilifungwa na Straika hatari wa TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samata, katika Dakika ya 90, kufuatia pande safi la Salum Abubakar lililompita kipa.
Taifa Stars ingeweza kufunga Bao mapema lakini Erasto Nyoni alikosa Penati katika Dakika ya 25 baada ya Kipa wa Cameroon, Komguep, kuicheza.
Penati hiyo ilitolewa kufuatia rafu kwa Samata.
Mechi hii ilikuwa ni ya kujijenga kwa Timu zote mbili ambazo Mwezi Machi zinakabiliwa na Mechi za Makundi ya Kanda ya Afrika kusaka kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil huku Tanzania ikiwa nyumbani kucheza na Morocco na Cameroon itacheza na Togo.
VIKOSI:
TAIFA STARS: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Aggrey Morris, Salum Abubakar, Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Mwinyi Kazimoto/Thomas Ulimwengu na Amri Kiemba.
CAMEROON: Effala Komguep, Bonnoit Assou-Ekotto, Aminou Bouba, Mgoula Patrick, Nyom Allan, Pierre Wome, Kingue Mpondo, Bedimo Henri/ Ashu Clovis (dk.73), Tchami Herve/ Elundu (dk.57), Olinga Fabrice/ Makoun Thierri (dk. 68) na Aboubakar Vincent/ Bakinde Gerrard (dk. 85).

No comments:
Post a Comment