Katika mpambano huo, Ivory Coast ndiyo iliyokuwa
ikipewa nafasi zaidi kufuatia kikosi chake kusheheni majina makubwa
kama vile Didier Drogba, Yaya Toure, Emmanuel Eboue, Gervihno, Kolo
Toure, Cheick Tiote, Salomon Kalou na wengine wengi ndiyo yaliyowapa
mashabiki wa timu ya Ivory Coast matumaini ya kusonga mbele.
Ivory
Coast ilisawazisha bao hilo baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na
Didier Drogba na kumfikia mfungaji Cheick Tiote katika dakika ya 51 na
kuunganisjha kwa kichwa mpira huo.
Hata hivyo Nigeria ilipata bao lingine la pili
katika dakika ya 78 likifungwa na Sunday Mba. Kosa la safu ya ulinzi ya
Ivory Coast kumwaachia mfungaji kukokota mpira kwa muda mrefu ndiko
kulikopeleka kilio kwa vijana wa Ivory Coast.
Kikosi cha Ivory Coast ambacho kilionekana kuwa
ni bora zaidi katika michuano hii, kimeonekana kuendelea na mkosi wake
kama ilivyokuwa mwaka jana wakitolewa katika fainali na Zambia, timu
ambayo haikupewa nafasi.
Wachezaji wengi wa Ivory Coast kama vile Didier
Drogba, Kolo Toure, Zokora na wengine wenye majina makubwa , huenda
mashindano haya yalikuwa ya mwisho katika kuchezea timu yao ya taifa,
kwani watakuwa na umri mkubwa na hivyo kutoshiriki michezo kama hii
mwaka 2015.
Mchezo unaofuata ni kati ya Burkina Faso na Togo
kukamilisha michezo ya robo fainali. Timu zilizosonga mbele ni pamoja
na Ghana, Mali na Nigeria, huku timu ya nne ikitoka katika mpambano kati
ya Burkina Faso na Togo.
No comments:
Post a Comment