BUKOBA SPORTS

Saturday, February 9, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: CHELSEA 4 vs WIGAN 1

CHELSEA 4 vs WIGAN 1
Frank Lampard kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa bado angali mmoja wa wachezaji wa kutegemewa wa Chelsea pale alipoiongoza timu yake kuilaza Wigan kwa magoli manne kwa mmoja, na kumaliza ukame wa Chelsea wa kutoshinda katika mechi nne mfululizo.
Ushindi huo sasa umemuondolea kocha wa Chelsea Rafael Benitez mzigo aliokuwa nao.
Lampard alifunga bao la tatu la Chelsea na kwa sasa anakaribia rekodi iliyowekwa na Boody Tambling ambaye aliifungia Chelsea jumla ya magoli 202.
Ramireza aliifungia Chelsea bao lake la kwanza kabla ya Edin Hazard kufunga bao la pili.
Kufikia wakati wa mapunziko Chelsea ilikuwa kifua mbele kwa magoli mawili kwa yai.
Katika kipindi cha pili Shaun Maloney alifufua matumaini ya Wigan kwa kuifungia bao hilo.
Lakini juhudi zao zilionekana kugongwa mwamba pale Lampard alipoongeza la tatu kisha Marko Marin kuongeza la nne.
Ushindi huo sasa umeisukumu Chelsea hadi nafasi ya tatu mbele ya Tottenham.
Ramires Akiifungia Chelsea goli la kwanza dhidi ya WiganRamires akishangilia baada ya kuifunga Wigan
Wachezaji wa Chelsea wakipongezana baada ya Hazard kuipatia goli
Marko Marin akishangilia baada ya kuifungia goli la kwanza kwa Chelsea dakika za lala salamaFernando Torres na Paul Scharner
James McArthur akichuana kuchukua mpira kutoka kwa David Luiz
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill (Benayoun 88), Cole, Luiz, Ramires, Oscar (Mata 77), Lampard, Hazard (Marin 90), Torres. Subs not used: Turnbull, Ferreira, Ba, Bertrand.
Booked: Marin.
Goals: Ramires 23, Hazard 56, Lampard 86, Marin 90.
Wigan: Al Habsi, Stam (Jones 83), Scharner, Caldwell, Figueroa, McCarthy, McArthur, Beausejour, Espinoza (Kone 59), Maloney, Di Santo. Subs not used: Robles, Henriquez, Gomez, McManaman, Golobart.
Booked: Scharner, Figueroa.
Goal: Maloney 58.
Attendance: 41,562
Referee: Mike Dean.


RATIBA/MATOKEO
Jumamosi Februari 9
[Saa 9 Dak 45 Mchana]
Tottenham Hotspur 2 v Newcastle United 1
[Saa 12 Jioni]
Chelsea 4 v Wigan Athletic 1
Norwich City  0 v Fulham 0
Stoke City  2 v Reading 1
Sunderland 0 v Arsenal 1
Swansea City 4 v Queens Park Rangers 1
[Saa 2 na Nusu Usiku]
Southampton  3 v Manchester City 1
 

Jumapili Februari 10
[Saa 10 na Nusu Jioni]
Aston Villa v West Ham United
[Saa 1 Usiku]
Manchester United v Everton
Jumatatu Februari 11
[Saa 5 Usiku]
Liverpool v West Bromwich Albion 
 

No comments:

Post a Comment