Santi Cazorla ameifungia bao kunako dakika ya hamsini na kuisaidia Arsenal kujizolea alama tatu muhimu dhidi ya Sunderland.
Arsenal iliyokuwa ikicheza na wachezaji kumi pekee sasa inashikilia nafasi ya tano kwenye msururu wa ligi kuu.
Carzola alivurumisha kombora kali iliyowapita walinda lango wa Sunderland pamoja na mlinda lango wao, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Theo Walcott.
Carl Jenkinson alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia mchezaji wa Sunderland madhambi.
Sunderland hata hivyo haikutumia fursa hiyo kufunga, licha ya mashambulizo makali katika lango la Arsenal.
Jack Wilshere akikwatuliwa na mchezaji wa Sunderland midfielder Alfred N'Diaye
No comments:
Post a Comment