BUKOBA SPORTS

Sunday, February 10, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: SOUTHAMPON 3 vs MANCHESTER CITY 1.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Premier ya England, Manchester City wamenyolewa bila maji na Southampton kwa kunyukwa magoli matatu kwa moja katika mchuano mkali wa ligi kuu ya Premier.
Jason Puncheon ameifungia Southampton bao lake la kwanza kabla ya Steven David kuongeza la pili.
Lakini mabingwa hao watetezi walifufua matumaini yao kwa kufunga bao la pili kupitia kwa nyota wake Edin Dzeko.
Lakini vijana hao wa Southampton ambao wanashiriki katika ligi hiyo kwa mara ya kwanza, baada ya kupandishwa daraja msimu uliopita, walijiimarisha na kufunga bao la tatu baada ya mcheza kiungo wa Manchester City Gareth Barry kujifunga.
Juhudi za mabingwa hao watetezi za kusawazisha ziligonga mwamba pale wachezaji wa Southampton walipoendeleza mashambulio yao dhidi ya Manchester City.
Kufuatia ushindi huo muhimu, Southampton sasa imepanda hadi nafasi ya kumi na saba na alama 27, huku Manchester City ikisalia katika nafasi ya pili na alama hamsini na tatu alama tisa nyuma ya Manchester United ambayo bado ingali na mechi moja zaidi.
Katika mechi zingine Tottenham imeishinda Newcastle kwa magoli mawili kwa moja Norwich ikatoka sare ya kutofungana bao lolote na Fulham, Stoke city nayo ikaishinda Reading kwa mabao mawili kwa moja na Swansea ikainyesha QPR magoli manne kwa moja.
Jason Puncheon akiipatia Sunderland goli dakika ya 7

Hakunaga... Puncheon akishangilia kwa aina yake

Joe Hart akifungwa na Steven Davis goli la pili kwenye dakika ya 22

Nyavu....

Edin Dzeko ameifungia City na kufanya 2-1 kabla ya mapumziko

Garth Barry akijifunga

Nyavu zikitingishwa

Manchester United kama wataifunga Everton kesho wataitangulia pointi 12 City
 VIKOSI:
Southampton: Boruc, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Fox (Richardson 71), Cork, Schneiderlin, Steven Davis (Ward-Prowse 80), Puncheon (Lallana 61), Rodriguez, Lambert.
Subs not used: Kelvin Davis, Forren, Lee, Chaplow.
Booked: Lambert.
Goals: Puncheon 7, Davis 22, Barry (og) 48.
Man City: Hart, Zabaleta, Lescott (Kolarov 66), Javi Garcia, Clichy, Nasri (Milner 55), Yaya Toure, Barry, Silva (Maicon 73), Aguero, Dzeko.
Subs not used: Pantilimon, Sinclair, Rodwell, Yaya Toure.
Booked: Clichy, Yaya Toure.
Goals: Dzeko 39.
Att: 31,738
Referee: Martin Atkinson
 
 
 
RATIBA/MATOKEO
Jumamosi Februari 9
[Saa 9 Dak 45 Mchana]
Tottenham Hotspur 2 v Newcastle United 1
[Saa 12 Jioni]
Chelsea 4 v Wigan Athletic 1
Norwich City  0 v Fulham 0
Stoke City  2 v Reading 1
Sunderland 0 v Arsenal 1
Swansea City 4 v Queens Park Rangers 1
[Saa 2 na Nusu Usiku]
Southampton  3 v Manchester City 1
 

Jumapili Februari 10
[Saa 10 na Nusu Jioni]
Aston Villa v West Ham United
[Saa 1 Usiku]
Manchester United v Everton
Jumatatu Februari 11
[Saa 5 Usiku]
Liverpool v West Bromwich Albion 
  

No comments:

Post a Comment