BUKOBA SPORTS

Tuesday, February 12, 2013

ENGLISH PREMIER LEAGUE: LIVERPOOL 0 vs WEST BROM 2, BAADA YA STEVEN GERARD KUKOSA PENATI YA UTATA, LUKAKU NA MC AULEY WACHINJA MAJOGOO HAO ANFIELD!!

Liverpool wakiwa kwao Anfield jana walinyukwa mabao 2-0 na Timu ya West Bromwich Albion. Liverpool walicheza kwa kujituma sana na kukosa magoli mengi na kipindi cha kwanza kuisha bila timu yoyote kuziona nyavu za mwezake. Liverpool ambao Mwaka huu mambo yao hayaendi vizuri jana walikosa penati, Penati iliyopigwa na Steven Gerrard kipindi cha pili na hatimaye kipa wa West Brom Foster kuipangua. Mapema Jonjo Shelvey aliifungia Liverpool goli lakini refa wa pembeni akanyanyua kipendera na kudai Jonjo ameotea. Magoli hayo ya West Brom yalipatikana dakika za mwishoni goli la kwanza likifungwa na McAuley dakika ya 81 baada ya kupigwa kona na McAuley akaifungia timu yake kwa goli la kichwa ambalo liligonga posti juu na kuishilia nyavuni. Goli la pili la West Brom lilifungwa dakika za lala salama baada ya kuingia mchezaji wao matata kipindi cha pili na dakika ya 74 ya mchezo. Dakika ya 90 Lukaku akaziona nyavu za Liverpool kwa kuwatoka vizuri mabeki wa Liverpool. Ushindi huu umewapandisha West Brom nafasi ya 8 wakiwa na pointi 37 juu ya Liverpool ambao wapo nafasi ya 9 na alama zao 36.
Gareth McAuley akiipatia timu yake goli la kwanza baada ya kupigwa kona

Wachezaji wa West Brom wakimpongeza McAuley kwa goli la kwanza, ambalo alilifungwa kwa kichwa baada ya kona kupigwa.
Sealed: Romelu Lukaku added West Brom's second goal in injury-time
Romelu Lukaku akiongeza goli la 2 kwa West Brom kwenye dakika za lala salama
Sealed: Romelu Lukaku added West Brom's second goal in injury-time
Lukaku akipongezwa.
 Luis Suarez akilalamika eneo la penati baada ya kuangushwa
Suarez aliangushwa na Jonas Olsson na Steven Gerrard kupewa nafasi hiyo ya kupiga mkwaju huo wa penati lakini bila kutegemea shuti hilo lilidakwa na kipa Foster.
Gerrard akipiga penati hiyo
 Ooooh Gerrard..nimeikosa....
VIKOSI:
Liverpool: Reina, Johnson, Carragher, Agger, Jose Enrique, Lucas, Gerrard, Henderson (Sterling 60), Downing (Coutinho 78), Shelvey (Borini 60), Suarez.
Subs not used: Jones, Allen, Skrtel, Wisdom.
Booked: Suarez.
West Brom: Foster, Reid, McAuley, Olsson, Ridgewell, Yacob, Mulumbu, Dorrans (Lukaku 74), Morrison, Brunt, Long (Fortune 86).
Subs not used: Myhill, Rosenberg, Jones, Tamas, Thomas.
Booked: Reid, Ridgewell, Morrison, Brunt.
Goals: McAuley 81,Lukaku 90.
Attendance: 44,752
Referee: Jon Moss

No comments:

Post a Comment