MANCHESTER CITY 2 LIVERPOOL 2
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu England,
Manchester City, leo wakiwa kwao Etihad, wakitoka nyuma ka Bao 2-1,
wameambua sare ya 2-2 toka kwa Liverpool baada ya kusawazisha kwa Bao
safi la Sergio Aguero kufuatia makosa ya Kipa Pepe Reina kutoka Golini
bila mpango na sare hii imewafanya wazidi kujichimbia nafasi ya pili
wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara Manchester United.
Sergio Aguero leo amewanusuru Mabingwa
watetezi, Man City, kichapo walipokuwa kwao Etihad alipofunga Goli la
pili na la kusawazisha kufuatia kosa kubwa la Kipa wa Liverpool Pepe
Reina kutoka nje na mbali ya Goli kufuata mpira na kujikuta akinasa
huko na Aguero kufunga Bao zuri toka engo kali sana.
Man City walitangulia kupata Bao kupitia
Edin Dzeko kufuatia krosi ya James Milner na Liverpool kusawazisha kwa
Bao la Daniel Sturridge.
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard,
aliechia kigogo kikali cha Mita kama 20 na kuwapa Liverpool bao la pili
ambalo Aguero alisawazisha Dakika 5 baadae baada ya makosa ya Kipa
Reina.Mchezaji David Silva wa Manchester City akichuana na Luis Suarez wa Liverpool Daniel Sturridge akipongezwa na wenzake baada ya kuisawazishia timu yake na kufanya 1-1Manchester City Manager Roberto Mancini akipagawa baada ya kufungwa goli la pili nakufanya 2-1Edin Dzeko wa Manchester City akishangilia mara baada ya kuipatia City goli la kwanzaSteven Gerrard akiachia shuti kali na kuipatia Liverpool goli la piliSteven Gerrard akishangiliaEdin Dzeko na Sergio Aguero baada ya kufungwa goli la pili...Hoi...Sergio Aguero akijionea mpira ukiingia kwenye goli baada ya Reina kufanya makosa
Aguero (nyuma) akishangilia huku kipa Pepe Reina akisikitika kuponzwa kwa kutoka golini
VIKOSI:
Manchester City: Hart; Zabaleta, Nastasic (Kolarov 56), Lescott, Clichy; Milner, García, Barry (Nasri 88), Silva (Maicon 73); Dzeko, Agüero.
Subs not used: Pantilimon, Rodwell, Sinclair, Tevez.
Booked: Dzeko, Garcia.
Goals: Dzeko 23, Aguero 78.
Liverpool: Reina; Johnson, Carragher, Agger, Enrique (Skrtel 75); Gerrard, Lucas, Henderson; Downing, Sturridge (Allen 90), Suarez.
Subs not used: Jones, Wisdom, Shelvey, Sterling, Borini.
Booked: Henderson, Sturridge, Carragher, Gerrard.
Goals: Sturridge 29, Gerrard 73.
Att: 47,301.
Ref: Anthony Taylor.
RATIBA WIKI IJAYO
Jumamosi Februari 9
[Saa 9 Dak 45 Mchana]
Tottenham Hotspur v Newcastle United
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Wigan Athletic
Norwich City v Fulham
Stoke City v Reading
Sunderland v Arsenal
Swansea City v Queens Park Rangers
[Saa 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Manchester City
Jumapili Februari 10
[Saa 10 na Nusu Jioni]
Aston Villa v West Ham United
[Saa 1 Usiku]
Manchester United v Everton
Jumatatu Februari 11
[Saa 5 Usiku]
Liverpool v West Bromwich Albion
No comments:
Post a Comment