Burkina Faso hatimaye imekuwa
timu ya nne kufuzun kwa nusu fainali ya kuwania kombe la mataifa ya
Afrika baada ya kuilaza Togo kwa bao moja kwa bila, katika mechi ya
mwisho ya robo fainali.
Licha ya Togo kupigiwa upato kushinda, mechi
hiyo sawa na ilivyokuwa katika robo fainali ya kwanza dhidi ya Ivory
Coast na Nigeria, Burkina Faso ilifuzu kwa nusu fainali hizo.
Togo
itajilaumu sana kwa kupoteza mechi hiyo, baada ya wachezaji wake
kupoteza nafasi nyingi sana za kufunga wakati wa mechi hiyo.
Baada ya dakika tisini za kawaida kumalizika, hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzie hatua iliyopelekea mechi hiyo, kuongezwa muda zaidi.
Kunako dakika ya 105 Burkina Faso hatimaye ikapata goli kupitia mchezaji wake Jonathan Pitroipa.
Pitroipa alifunga bao hilo kwa kichwa kufuatia mpira wa kona.
Burkina Faso sasa itacheza na Ghana katika nusu fainali ya pili siku ya Jumatano mwendo wa saa mbili na nusu majira ya Afrika Mashariki.
Pitroipa alifunga bao hilo kwa kichwa kufuatia mpira wa kona.
Burkina Faso sasa itacheza na Ghana katika nusu fainali ya pili siku ya Jumatano mwendo wa saa mbili na nusu majira ya Afrika Mashariki.
Nusu Fainali ya kwanza itakuwa kati ya Nigeria na Mali.
Kwa mwaka mwingine tena timu zilizosalia kwenye
mashindano hayo, zinatoka Afrika Magharibi baada ya timu nyingine kutoka
maeneo ya Kaskazini, Mashariki na Kusini kubanduliwa nje ya michuano
hiyo.Burkina Faso wakishangilia
Emmanuel Adebayor anajipanga kurudi Spurs baada ya Togo kuondolewa kwenye mashindano.
Shujaa Jonathan Pitroipaakipongezwa na mashabiki wa Burkino Faso
Burkina Faso wakiomba baada ya kushinda kuingia nusu fainali baada ya kipindi kirefu tangu 1998
VIKOSI:
Burkina Faso: Diakite, Koffi, Keba Paul Koulibaly, Bakary Kone, Panandetiguiri, Djakaridja Kone, Ouattara (Nakoulma 66), Kabore, Wilfried Sanou (Abdou Razak Traore 96), Dagano, Pitroipa (Rouamba 109).
Subs Not Used: Soulama, Dah, Henri Traore, Balima, Bance, Rabo, Pan-Pierre Koulibaly, Germain Sanou.
Booked: Ouattara, Kabore.
Goals: Pitroipa 105.
Togo: Agassa, Mamah, Bossou, Nibombe, Djene, Amewou (Salifou 116), Akakpo (Wome 106), Romao, Gakpe, Adebayor, Floyd Ayite (Segbefia 67).
Subs Not Used: Atsu, Jonathan Ayite, Mani, Ouro-Akoriko, Placca, Ametepe, Donou, Damessi, Tchagouni.
Booked: Floyd Ayite, Gakpe, Mamah, Romao, Adebayor, Bossou.
Att: 27,000
Ref: Badara Diatta
No comments:
Post a Comment