KLABU ya Barcelona imedai kuwa mchezaji nyota wa kimataifa wa Ufaransa na klabu hiyo, Eric Abidal ameanza mazoezi ya moja kwa moja ikiwa ni miezi 10 imepita toka afanyiwe upasuaji wa kupandikiza ini jingine. Abidal ambaye alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe katika ini lake Machi mwaka 2011 kabla ya kurejea tena uwanjani katika mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester United, alikuwa nje ya uwanja toka alipofanyiwa upasuaji huo Aprili mwaka jana. Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 33 anaweza kujumuishwa katika kikosi cha Barcelona kinachonolewa na kocha msaidizi Jordi Roura ambacho kitapambana na Getafe katika mechi ya La Liga Jumapili.Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imeeleza kuwa baada ya nyota huyo kutumia siku kadhaa hospitali kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ini lake alilopandikizwa ameanza mazoezi rasmi. Roura amekabidhiwa timu hiyo baada ya kocha mkuu Tito Vilanova akiendelea na matibabu ya mionzi kwa ajili ya kupambana na kansa ya koo inayomkabili.
No comments:
Post a Comment