Jana Huko, Stamford Bridge, Sparta Prague walikuwa wakiongoza kwa Bao 1-0 na kufanya wafungane na Chelsea kwa Bao 1-1, Bao la Eden Hazard la Dakika ya 90 lilifanya Mechi iwe sare 1-1 na Chelsea kusonga kwa jumla ya Bao 2-1 katika Mechi mbili.
Awali, Tottenham na Newcastle, zilizokuwa zikicheza ugenini, zote zilifuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Tottenham ilitoka sare 1-1 na Lyon na Newcastle kuifunga Metalist Kharkiv 1-0.
Huko ANFIELD mambo yalikuwa magumu sana licha ya Suarez kung’ara kwa kupiga Bao 2 safi na kuipa Liverpool ushindi wa Bao 3-1 dhidi ya Zenit St Petersburg ambao Bao lao lilifungwa na Straika hatari Mbrazil Hulk, na hilo ndio Bao lililowaua Liverpool kwani baada ya Mechi mbili Mabao yalifungana kuwa 3-3 na Bao la ugenini la Hulk kuitupa nje ya EUROPA LEAGUE Liverpool.
Goli la Hulk liliwaua Liverpool mara mbili na kuwapandishia deni la magoli
Liverpool mpaka mapumziko walihitajika kufunga goli mbili ili kujihakikishia
Pia, waliokuwa Mabingwa watetezi wa
Kombe hili, Atletico Madrid, walibwagwa nje ya EUROPA LEAGUE licha ya
kuifunga ugenini Rubin Kazan Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 85 la Falcao,
kwa vile walifungwa 2-0 katika Mechi ya kwanza.
Kabla ya Mechi hizi za Raundi hii, kila
Timu ilikuwa ikijua nani atakuwa mpinzani wake endapo wakitinga Raundi
ya Mtoano ya Timu 16.
Shola Ameobi akishangilia.
FC Metalist Kharkiv's mashabiki walikuwa nongwa kwa timu ya Newcastle, kelele nyingi zikiandamwa na usumbufu wa hapa na pale ... lakini Newcastle waliweka pamba masikioni na kuendelea na mtanage na hatimaye kuibuka na ushindi jana usiku kwenye Europa ligi.
RAUNDI IJAYO: KUCHEZWA MACHI 7 na 14
EUROPA LEAGUE LAST-16 DRAW
Anzhi Makhachkala vs Newcastle
Basle vs Zenit St Petersburg
Benfica vs Bordeaux
Levante vs Rubin Kazan
Steaua Bucharest vs Chelsea
Stuttgart vs Lazio
Tottenham vs Inter Milan
Viktoria Plzen vs Fenerbahce
EUROPA LEAGUE LAST-16 DRAW
Anzhi Makhachkala vs Newcastle
Basle vs Zenit St Petersburg
Benfica vs Bordeaux
Levante vs Rubin Kazan
Steaua Bucharest vs Chelsea
Stuttgart vs Lazio
Tottenham vs Inter Milan
Viktoria Plzen vs Fenerbahce
No comments:
Post a Comment