Kwa mara nyingine matumaini ya
klabu ya Arsenal, kumaliza ukame wa miaka zaidi ya saba ya bila
kunyakuwa kikombe chochote yamepotea mchana wa leo,baada ya kupoteza
mchezo wao wa marudiano dhidi ya klabu ya iliyoshuka daraja msimu
uliopita, Blackburn Rovers.
Lilikuwa ni shuti kali la Martin Olsson's ambalo
lilimshinda kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny na kuzaa bao pekee
lililofungwa na Colin Kazim-Richards kunako dakika ya 72 ya mchezo huo
uliokuwa ukifanyika kwenye uwanja wa Emirates ndilo liliiwezesha
Blackburn kuondoka na ushindi ugenini.
Kwa mara nyingine matumaini ya
klabu ya Arsenal, kumaliza ukame wa miaka zaidi ya saba ya bila
kunyakuwa kikombe chochote yamepotea mchana wa leo,baada ya kupoteza
mchezo wao wa marudiano dhidi ya klabu ya iliyoshuka daraja msimu
uliopita, Blackburn Rovers.
Arsenal
wameshindwa kutwaa taji lolote kubwa kwa miaka zaidi ya saba,ambapo
msimu huu wamekuwa na matumaini ya kufika mbali kwenye michuano ya kombe
la FA jambo ambalo leo limeshindwa kutimia baada ya kuondolewa na
Blackburn.Matokeo ya leo yameifanya Arsenal kwa mara ya pili kuondolewa kwenye michuano mikubwa na klabu ndogo,ambapo mapema msimu huu waliondolewa kwenye Bradford kwenye kombe la ligi.
Kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini England,Arsenal wanakamata nafasi ya tano nyuma ya Tottenham wakiwa na point 44.Francis Coquelin akifanya mambo yake.Gervinho na Lee Williamson (kulia) wakikabana usiku jioni hii kwenye FAmchezaji wa Blackburn Rovers Colin Kazim-Richards akiruka juu kugombea mpira
Mashine zikiingia - Jack Wilshere (kushoto), Theo Walcott (katikati) na Santi Cazorla (kulia)
Kazim-Richards akiruka juu kushangilia goli lake ambalo limedumu mpaka mwisho
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Vermaelen, Koscielny, Monreal, Diaby, Rosicky (Wilshere 70), Arteta, Oxlade-Chamberlain (Cazorla 70), Coquelin, Giroud, Gervinho (Walcott 70)
Subs not used: Mannone, Sagna, Ramsey, Podolski
Booked: Coquelin
Blackburn: Kean, Orr, Martin Olsson, Dann, G Hanley, Lowe, Pedersen, Marcus Olsson (Bentley 63), Williamson, Rhodes (Goodwillie 83), Kazim-Richards
Subs not used: Usai, Givet, Rekik, Nunes, Nuno Gomes
Booked: Orr, Goodwillie
Goal: Kazim-Richards 72
Referee: Mike Dean
Attendance: 60,070
No comments:
Post a Comment