Tuesday, February 12, 2013

OMOTOLA JALADE AVUNJA REKODI NIGERIA


Mwigizaji mahiri wa filamu nchini NIGERIA amevunja rekodi kubwa ambayo inathibitisha kuwa ana mashabiki wengi mitandaoni na hii ni baada ya kuwa mtu maarufu wa kwanza wa nchi hiyo kuwa na mashabiki zaidi ya milioni moja katika ukurasa wake wa facebook pekee.
Kwa sasa idadi kamili ya watu ambao wamependa ukurasa wa mwanadada huyu ni 1,001,822 na bado mashabiki wake wanaendelea kuongezeka kwa kasi kutokana na mwanadada huyu kufanikiwa kuongeza wigo wa fani zake ndani ya muziki, filamu na vipindi vya televisheni.
Hii ni kama zawadi kubwa kwa Omotola ama Omosexy kama anavyopenda kufahamika hasa katika kusherekea kutimiza miaka 34 tangu kuzaliwa kwake Februari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment