Msako wa kukamata kazi za wasanii umefanyika mkoani hapa Kagera katikati ya wiki hii na Hatimaye kumtia nguvuni mhusika wa kazi hiyo chafu inayorudisha nyuma maendeleo ya wasanii wetu hapa nchini Tanzania.
Bw. MUMBE MARTINE Raia wa Uganda ambaye alikuwa humu Bukoba kwa kazi hiyo
ya kuuza kazi za Sanaa kama vile Filamu na
nyimbo za wasanii Watanzania
zilizodurufiwa kinyume na sheria haki miliki na haki Shiriki.

Bwana Mumbe Martine(30) alikamatwa Mkoani Kagera tarehe 15.02.2013 majira
ya saa saba na dakika 13 (1:13) mchana maeneo ya Hamugembe mkoani hapa akiwa na
kazi hizo (DVD pamoja na CD) jumla zikiwa 90. Ambazo ni kazi za wasanii
mbalimbali zikiwemo na za wasanii wa hapa nchini.
CD Hizo Zikiwemo za Steps
Entertainment na za Msama Production. Kama Radhi au Penzi part 2, Millosis,
Damage, The Shell na Doctor wa Kifimbo pamoja na kazi za
Solomoni Mkubwa na n.k.

No comments:
Post a Comment