BUKOBA SPORTS

Sunday, February 17, 2013

LA LIGA: GRANADA 1 vs BARCELONA 2

Bao 2 za Lionel Messi jana ziliwapa ushindi wa ugenini Vinara wa La Liga, Barcelona, walipoifunga Granada Bao 2-1.
Granada ndio walitangulia kufunga kwa Bao la Ighalo katika Dakika ya 26 lakini Bao za Kipindi cha Pili za Messi, Dakika ya 50 na 73, ziliwapa ushindi Barcelona na kuwafanya wafikishe Pointi 65 huku Timu ya Pili, Atletico Madrid ikiwa na Pointi 50 wakifuatiwa na Real Madrid wenye 46 lakini Atletico na Real wana Mechi moja mkononi ambazo wanacheza leo.Na zaidi, Messi ameendeleza rekodi yake ya kufunga katika mechi 14 mfululizo na ni mchezaji wa kwanza katika historia ya 'La Liga' kufunga katika mechi 10 mfululizo za ugenini.

Messi hivi sasa anaongoza 'ligi' ya wafungaji wa 'La Liga' akiwa na magoli 37, yanayomweka katika nafasi nzuri ya kuivunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka mwaka jana ya kufunga magoli 50 katika Ligi Kuu, hasa ukizingatia kwamba kuna mechi 14 bado za kucheza hadi mwisho wa msimu.
Messi akitupia..
Lionel Messi akipita katikati ya mabeki wa Granada
 Lionel Messi akifunga goli la pili

Messi akishangilia goli lake la pili pamoja na wachezaji wenzake jana usiku



No comments:

Post a Comment