BUKOBA SPORTS

Thursday, February 14, 2013

TANZANIA YASHUKA NAFASI 3 KWENYE VIWANGO VYA SOKA DUNIANI, SPAIN ADO WAPO NAFASI YA KWANZA.

Katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa leo, Mabingwa wa Dunia, Spain, bado wanashikilia Namba moja wakifuatiwa na Germany, Tanzania imeshuka nafasi 3 na sasa ipo nafasi ya 127 licha ya kuifunga Cameroun Bao 1-0 hivi majuzi.
England, kwa kuifunga Brazil, wamepanda hadi nafasi ya 4 huku Ivory Coast ndio Timu toka Afrika iliyo juu kabisa ikiwa nafasi ya nafasi ya 12 baada ya kupanda nafasi kadhaa.
Mabingwa wapya wa Afrika, Nigeria, wamepanda nafasi 22 na sasa wapo nafasi ya 30 na Timu waliyoifunga Fainali, Burkina Faso, imepanda nafasi 37 na wapo nafasi ya 55.
Listi nyingine ya FIFA ya Ubora Duniani itatolewa Mwezi ujao hapo Machi 14.
TOP TEN:
1. Spain
2. Germany
3. Argentina
4. England
5. Italy
6. Colombia
7. Portugal
8. Netherlands
9. Croatia
10. Russia

No comments:

Post a Comment