Wachezaji wa simba, wakimpongeza kiungo wao Mwinyi Kazimoto, baada ya kuifungia timu yake bao, wakati wa mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha loe jioni. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 1-1.
*********
TIMU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo jioni imevutwa shati na JKT Oljoro baada ya kufungana bao 1-1, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Voidacom Tanzania Bara, mzunguko wa pili uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Kwa timu ya Simba leo imetimiza sare ya pili tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo, baada ya wiki iliyopita kulazimishwa sare kama hiyo na JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaamm na kuifanya
Simba kutimiza jumla ya pointi 28, baada ya kucheza mechi 16, huku watani wao Yanga wakiongoza kwa kuwa na pointi 33 na mchezo mmoja mkononi, wakati Azam FC ya pili wakiwa na pointi 30 na mchezo mmoja mkononi.
Bao la JKT Oljoro, lilifungwa na Paul Nonga, katika dakika ya tisa tu tangu kuanza kipindi cha pili.
No comments:
Post a Comment