BUKOBA SPORTS

Sunday, February 10, 2013

ROBERTO MANCINI: MATUMAINI YA UBINGWA YAMEBAKI ASILIMIA 10

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini amedai kuwa kipigo cha mabao 3-1 ambacho timu imepokea kutoka Southampton kinaaminisha kuwa nafasi yao ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza imebakia asilimia 10 pekee. MENEJA wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini amedai kuwa kipigo cha mabao 3-1 ambacho timu imepokea kutoka Southampton kinaaminisha kuwa nafasi yao ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza imebakia asilimia 10 pekee. Vinara wa ligi hiyo Manchester United wanaweza kuongeza pengo dhidi ya City wanaoshika nafasi ya pili kufikia alama 12 huku kukiwa kumebakia michezo 12 kabla ya kufikia ukingoni kama timu hiyo ikishinda mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Everton baadae leo.Vinara wa ligi hiyo Manchester United wanaweza kuongeza pengo dhidi ya City wanaoshika nafasi ya pili kufikia alama 12 huku kukiwa kumebakia michezo 12 kabla ya kufikia ukingoni kama timu hiyo ikishinda mchezo wake wa nyumbani dhidi ya Everton baadaye leo. City ilifanikiwa kutengeneza alama nane katika michezo sita
iliyobakia msimu uliopita na kufanikiwa kuinyang’anya United taji la ligi hiyo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Lakini msimu huu Mancini anafikiri nafasi yao ya kutetea taji lao imebaki kidogo kufikia asilimia 10 pekee na hadhani kama United wanaamini wanaweza kuliziba pengo hilo la alama 12.

No comments:

Post a Comment