BUKOBA SPORTS

Friday, March 29, 2013

BREAKING NEWS: JENGO LA GHOROFA 16 LAPOROMOKA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU KADHAA JIJINI DAR LEO HII.

Jengo la ghorofa 15 limeporomoka katikati ya Jiji la Dar es laam, watu 17 wameokolewa na wawili(2) wamepoteza maisha na Kazi ya kuokoa inaendelea.....
Inasadikiwa bado kuna maiti za watu zimefukiwa na kifusi.

Mtoto Maisamali Karim (6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Jamaat iliyoangukiwa na jengo hilo katika mtaa wa Indira Gandhi. (Picha zote na Habari Mseto Blog)

Changamoto ya uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo, ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.

Hizi nia aina ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho kampuni za ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo hayo.

Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la uokoaji likiendelea.

Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.

Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA JENGO LILILOPOROMOKA DAR ES SALAAM LEO


Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadcik akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said cMeck Sadick shoto akiwa ameambatana na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge,Mh Mbatia muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya.,aidha shughuli za ukoaji zinaendelea kwani inadaiwa kuna watu wengi zaidi wamefunikwa na jengo hilo.

Rais Kikwete akiondoka eneo la tukio mara baada ya kujionea hali halisi ya tukio zima la kuanguka kwa ghorofa linalodaiwa kuwa na idadi ya ghorofa 16.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akifafanua jambo kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.Dkt.ASha-Rose Migiro kuhusiana na tukio zima la kuanguka kwa jengo la Ghorofa mapema leo asubuhi,jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akipewa pole na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.Dkt.ASha-Rose Migiro kuhusiana na tukio zima la kuanguka kwa jengo la Ghorofa mapema leo asubuhi,jijini Dar.
Wadau wakimwagia maji kijiko cha greda ili kurahisisha kuingia kwenye kifusi.

Wanajeshi wakiendelea na kazi ya uokoaji.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.

Waokoaji.





Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP), Suleima Kova kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka majira ya saa mbili asubuhi katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo. (Picha zote na Habari Mseto Blog)

Waokoaji wakiwa kazini.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova akiwa katika eneo la tukio. Kulia ni Mbunge wa viti maalum (NCCR-Mageuzi James Mbatia.

No comments:

Post a Comment