Bobby Williamson ametimuliwa kibarua cha kuinoa timu hiyo baada ya kuifundisha kwa miaka minne na miezi nane. Shirikisho la Soka la nchi hiyo-FUFA lilithibitisha kumtimua Bobby Williamson katika kikao cha dharura walichokutana ingawa hakuna sababu haswa zilizotajwa ambazo zimepelekea kumtupia virago kocha huyo. Wlliamson mwenyewe alipotafutwa kuthibitisha taarifa hizo kwa njia ya simu alikubali kuwa ni kweli ameshapata barua ya kusitisha mkataba lakini alikataa kuongelea undani suala hilo akidai bado ni mapema. Kuhusu nani atachukua nafasi ya kocha huyo ofisa habari wa FUFA, Rogers Mulindwa amewaambia waandishi wa habari kuwa suala hilo litatuliwa na kamati ya utendaji itakapokutana ingawa hakuweka wazi ni lini haswa kamati hiyo itakaa.
Monday, April 8, 2013
UGANDA WAMTIMUA KOCHA BOBBY WILLIAMSON THE CRANES.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment