Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akionesha aina mpya ya Smart Phone wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Bando na TTCL na kampeni ya punguzo kubwa la bei ya intaneti uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mauzo TTCL, Kisamba Tambwe. (Picha na Habari Mseto Blog)
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akizindua Huduma ya Bando na TTCL na kampeni ya punguzo kubwa la bei ya intaneti uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Bidhaa TTCL, Issaya Ernest.
KAMPUNI ya simu Nchini (TTCL) leo imezindua huduma mpya ya Bando na TTCL itakayomuwezesha mteja kufaidika na meseji bila kikomo ,kuperuzi intaneti na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa bei nafuu.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu Ofisa Mkuu wa Mauzo Peter Ngota alisema huduma ya bando na TTCL itamuwezesha mteja pia kutuma meseji bila kikomo kwa bei ya hadi shilingi mia tano.
Alisema bando TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za kisasa za smart phones za kampuni hiyo ambazo zinapatikana katika vituo vyao vya simu kote nchini.
Alisema kampuni hiyo imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile internet kwa kampeni ya Basti ikimaanisha peruzi internet zaidi kwa gharama nafuu.
“Hii ni punguzo la bei la aina yake , mathalani kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa shilingi 90,000 sasa kinauzwa shilingi 25,000 hii ni nafasi sit u kwa wateja waliopo TTCL kuongeza matumizi kwa gharama nafuu bali hata kwa wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga na mtandao wa TTCL,”alisema Ngota.
Alisema Bando na TTCL na kampeni ya Basti zina manufaa kkwa mteja ikiwa ni pamoja na huduma ya mobile internate kwa gharama nafuu,vifurushi vya siku ,wiki na mwezi kulingana na mahitaji ya mteja,mobile internate yenye ubora na kasi ya juu zaidi,kwa kununua modemu ya shilingi 29,900 utapata 2GB bure kuperuzi intaneti.
Aidha alisema kua huduma ya bando na TTCL inapatikana pia kwa simu za kisasa za smart phones na inatoa thamani bora kwa pesa huku akieleza kua kama kampuni kongwe na mhimili wa mawasiliano nchini inatambua kuwa na jukumu kubwa la kutoa huduma za mawasiliano kwa wateja kote nchini.
No comments:
Post a Comment