BUKOBA SPORTS

Thursday, April 4, 2013

MWAMUZI MTATA NA MZOEFU "MIKE DEAN" KUCHEZESHA MPAMBANO WA UNITED NA CITY JUMATATU TAREHE 8.4.2013

JUMATATU USIKU APRILI 8 upo mtanange mkali kati ya Mahasimu wakubwa wawili wa JijiniManchester, Vinara wa BPL, Barclays Premier League, Manchester United na Mabingwa watetezi Manchester City ndani ya Old Trafford na Mechi hii, licha ya Man United kuwa Pointi 15 mbele ya City huku Mechi zikibaki 8, ndio inayotamkwa kuwa itatoa Bingwa wa BPL Msimu huu na imekolezwa na uteuzi wa Refa ambae kila upande una wasiwasi naye.
Refa huyu si mwingine ila ni mmoja wa Marefa wazoefu sana kwenye BPL, Mike Dean.
Mara kadhaa Dean ameshawahi kuvurugana na Meneja wa Man United Sir Alex Ferguson na pia Meneja wa Man City Roberto Mancini.

Mara ya mwisho kwa Mike Dean kuichezesha Man United ni hapo Desemba 26 wakati Man United ilipoifunga Newcastle Bao 4-3 na Ferguson kumvaa Refa huyo wakati wa Haftaimu kwa kukubali goli la utata la Newcastle la kujifunga mwenyewe Jonny Evans.

Naye Bosi wa Man City, Roberto Mancini, alikasirishwa pale Refa Mike Dean alipomtoa nje Nahodha wake Vincent Kompany walipoifunga Arsenal Bao 2-0 Mwezi Januari lakini City waliikatia Rufaa Kadi hiyo na FA ikaifuta.
...Nimesema nje...ujaja kunifundisha kazi mie..

No comments:

Post a Comment