Toure, mwenye Miaka 29, amekuwa nguzo kubwa kwa Man City tangu ajiunge hapo Mwaka 2010 kwa Dau la Milioni 24 akitokea Barcelona.
Katika Msimu wake wa kwa kwanza na City, Klabu hiyo ilitwaa FA CUP Mwaka 2011 na Mwaka uliofuatia walitwaa Ubingwa wa England.
Pia Toure ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Miaka ya 2011 na 2012.
Baada ya kusaini Dili hii mpya, Toure alitamka: “Hapa ndipo ninapotaka kuwepo! Nilipotua City kwa mara ya kwanza, kila nikilala nilikuwa naota sisi tumetwaa Taji fulani! Sasa ni zamu yetu kuwa bora katika kila Mashindano tunayoshiriki!”
Yaya Toure amekubali mwenyewe kuendelea kuichezea Citykwa miaka minne
No comments:
Post a Comment