BUKOBA SPORTS

Tuesday, July 2, 2013

KAMA ULIKOSA TAMASHA LA TIGO MINI KABANG JIJINI MWANZA ANGALIA TUKIO ZIMA HAPA!

Mashabiki wa Jiji la Mwanza kutoka mtaa mmoja hadi mwingi walikusanyika uwanja wa ccm Kirumba kama sehemu ya kujuika pamoja na issue nzima ya Tigo Mini Kabang hapa!





CCM KIrumba palikuwa hapatoshi!!

Mashabiki wa tigo Mini Kabang

Mshindi wa simu ya mkononi kutoka Tigo Bw. Faraji Ismail (kushoto) akipungia simu aliyoshinda na kuzawadiwa na mwakilishi wa Tigo kanda ya ziwa Bw. Eliud Mjuni (kulia). Katikati ni MC Nambiles Msimbe.
Msanii Madee anayetamba na kibao ‘Nani kamwaga pombe yangu’ akitoa burudani.

Msanii bora wa mwaka Naseeb Abdul aka Diamond au Rais wa Wasafi akitoa burudani pamoja na kundi lake la Wasafi.
Wasafi nao wakalipuka!!!



Ni kama Staili ya aina yake na ya kipekee sana kwa wasafi!!!







Msanii Recho juu ya stage akiwapagawisha mashabiki wa Mwanza.

Umati wa mashabiki wa Mwanza waliofika katika tamasha la Tigo Mini Kabaang katika viwanja vya CCM Kirumba.

Nje ya Mwanza wanamfahamu kama Fid Q lakini kwao jijini Mwanza washamzoea kama Farid Kubanda. Hapa alikuwa aki-rock city ya Mwanza ndani ya tamasha la Tigo Mini Kabaang.
Fid Q naye akiwapa raha wakazi wa Mwanza, na kabla ya kuanza alikaribishwa kwanza nyumbani ...kisha akalisanua mwanzo mwisho!!!

Kikundi cha Jackson 5 kutoka Mwanza wakipafomu nyimbo yao ‘Maishani’ inayotamba jijini humo.

Msanii Ney wa Mitego (katikati) akishuka kutoka kwenye gari la Tigo tayari kwa kuwaburudisha mashabiki wa Mini Kabaang jijini Mwanza.

‘Kidole cha mwisho juu’ hiyo ndiyo ilikuwa sauti ya umati mzima pale msanii Roma Mkatoliki alivyopanda jukwaani kuwaburudisha maelfu ya mashabiki waliofurika katika tamasha la Tigo Mini Kabaang viwanja vya CCM Kirumba. Roma Mkatoliki akipagawisha mashabiki wake

Dj akikandamiza na kusababisha hapa vitu viende safiiii!!

Roma Mkatoliki akifoka foka!!..

ROMA akiwasha Moto CCM Kirumba

Rich Mavoko akipafomu nyimbo ya ‘Mapenzi Sukari’ katika tamasha la Tigo Mini Kabaang.

No comments:

Post a Comment