BODI MISS UTALII TANZANIA YAFANYA MAAMUZI MAGUMU.
Yasimamisha shindano kwa mwaka mmoja
Bodi ya taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO), yenye dhima ya kikomo ya kuratibu na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imetangaza kusimamisha kufanyika mashindano hayo katika ngazi zote kwa msimu wa 2013/2014. Lengo la kutofanya mashindano hayo kwa mwaka mmoja ni kujipanga upya na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa mashindano katika ngazi zote.
Bodi ya taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO), yenye dhima ya kikomo ya kuratibu na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imetangaza kusimamisha kufanyika mashindano hayo katika ngazi zote kwa msimu wa 2013/2014. Lengo la kutofanya mashindano hayo kwa mwaka mmoja ni kujipanga upya na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa mashindano katika ngazi zote.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT SAADANI NATIONAL PARK
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo Erasto Gideon Chipungahelo, uamuzi huo mgumu umechukuliwa na bodi ya mashindano hayo wakati wa kikao cha tathimini ya miaka mitano ya mashindano hayo, na miaka kumi ya taasisi ya Miss Tourism Tanzania Organisation ambayo ilisajiliwa na kuanzishwa rasmi mwaka 2002,sambamba na usajili wa mashindano hayo. Fainali za kwanza za Miss Utalii Tanzania, zilifanyika mwaka 2004katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam, na fainali za tano za Miss Utalii Tanzania zilifanyika Mei 19,2013 katika uwanja wa mkwakwani Tanga.
Bodi
katika tathimini hiyo ya ndani imebaini changamoto mbalimbali za kimfumo,udhamini,
utendaji,kuporomoka au kudumaa kwa sanaa ya urembo nchini na hujuma. Mfumo DUME
wa uendeshaji wa mashindano ya urembo nchini kikwazo kwa ukuaji wa wazo au
ubunifu wa kazi ya sanaa husika, kwani bodi imebaini mfumo huo kutoa mianya ya hujuma na kupindishwa kwa
wazo na lengo mama la mbunifu.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT WAMI RIVER SAADANI NATIONAL PARK |
Lakini
pia mfumo DUME wa udhamini, umekuwa ni kikwazo na changamoto kubwa kwa ukuaji
wa sanaa nchini, kwani mfumo uliopo wa udhamini unatoa fulsa ya wadhamini kuwa
wafalme au miungu watu , kiasi cha kudhamini kisicho bora,kisicho na mafanikio,
kisicho na tija katika jamii na kuacha kudhamini kilicho bora,chenye tija
katika jamii na kilicho na mafanikio makubwa kitaifa na kimataifa. Kwa
visingizio na sababu mbalimbali mfumo wa udhamini nchini umekuwa ukitoa fulsa
kwa wadhamini kuwa waandaaji na kupotosha kabisa maudhui ya ubunifu wa sanaa
husika. Mfumo wa udhamini nchini umezaa aina mpya ya Utumwa wa kujitumikisha na
kuwafanya wabunifu wa kazi za sanaa kuwa watwana na wadhamini kuwa mabwana
mkubwa.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT SAADANI NATIONAL PARK |
Kwa
zaidi ya miaka 18 sasa tangu kuanza upya kwa sanaa ya urembo nchi, tumeshudia
kuanzishwa na kufa au kuuawa kwa mashindano na kazi mbalimbali za ubuni fu wa
sanaa hii. Aidha katika kipindi hiki tumeshudia kuporomoka kwa kasi ya ajabu
kwa sanaa ya urembo nchini,tofauti na nchi jirani na nyinginezo duniani. Kuporomoka
ambako kumepelekea umaarufu wa matamasha ya urembo nchini kuporomoka. Zipo
sababu nyingi za kuporomoka kwa sanaa hii nchini, chache kati ya hizo ni Mfumo
DUME wa Udhamini, kutotambua unyeti wa taaluma ya sanaa ya urembo kuwa ni wazo
na ubunifu wa mtu kwa msukumo nafsi wa mtizamo,fikra na imani ya kuamini katika
ndoto yake. Hii inamaana kuwa tofauti na michezo au sanaa nyingine sanaa ya
urembo hususani mashindano ya urembo hayana fomila wala mfumo yakini, kama
ilivyo kwa mpira wa miguu,au muziki au uigizaji wa filamu, uchezaji na upigaji
wa ngoma za asili n.k, hivyo kwa kiasi kikubwa hutegemea ubunifu na mtizamo wa
mbunifu wa shindano husika katika kufikia ndoto ya ubunifu na matarajio yakea
juu ya wazo husika.
MISS TOURISM TANZANIA 2013, AT SAADANI NATIONAL PARK
Bodi
imebaini kuwa mifumo ya uendeshaji iliyopo inatoa mianya ya hujuma baina ya
shindano na shindano na hata baina ya wadhamini wa shindano flani na
jingingine, lakini pia baina ya wabubunifu na mafisadi wa kazi za sanaa za
wabunifu wajasilia mali.Hapa hujuma zimegawanyika katika makundi tofautitofauti
ikiwemo waraembo mamluki wanao pandikizwa katika mashindano mengine, viongozi
au wajumbe wa kamati mamluki na wale wenye uchu wa madaraka na kuvuna bila ya
kupanda, lakini hujuma kupitia propaganda chafu, fitina,majungu na kupakana
matope. Zipo hujuma pia za watu wa kada mbalimbali katika jamii kutumiwa
kufanikisha adhma ya mafisadi wa kazi za ubunifu wa sanaa na upindishaji wa
sheria na taratibu za uendeshaji wa mashindano ya urembo duniani na sanaa nzima
ya urembo kitaifa na kimataifa.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT DAR ES SALAAM UNIVERSITY (SJM) |
Udhamini
na hujuma imekuwa ni changamoto kubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa mashindano
haya ya Miss Utalii Tanzania. Tofauti na mtizamo wa wengi kuwa tumekuwa
tukipata udhamini na wadhamini wakubwa katika Miss Utalii Tanzania , ukweli ni
kwamba hakuna udhamini wowote mkuu na mkubwa tunao upata kutoka kwa sekta
binafsi wala ya umma, badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali zetu na nguvu
zetu kufanikisha kufanyika kwa fainali za kila mwaka , ikiwemo kugharamia
ushiriki wa washindi wa Taifa katika mashindano ya Dunia , japo katika
mashindano yote 6 ya Dunia na mengineyo ya kimataifa tume peperusha vyema
bendera ya Taifa na Utalii wa Tanzania
kwa kutwaa mataji katika mashindano yote tuliyo shiriki, tunashikilia zaidi ya
mataji 7 ya Dunia hadi sasa.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 CONTESTANTS |
Mafanikio
haya ya kimataifa matunda yake ni pamoja na Tanzania kupewa heshima ya kuwa
wenyeji wa fainali za Dunia za Miss Tourism World 2006. Fainali ambazo kwetu
zimekuwa kama mwiba wa mchongoma kutokana na watu wengi kudhani kuwa udhamini
tulio upata wa serikali ulikuja kwetu, wakati ukweli ni kwamba fedha zili
zilikwenda Miss Tourism World Organisation na kulipa watoa huduma wa ndani
walio hudumia huduma mbalimbali zikiwemo za malazi, chakula, usafiri,
matangazo, ulinzi, kumbi, taa na majukwaa.
Ni
kama mwiba wa mchongoma kwetu kwa sababu, wengi wanadhani na kuamini kuwa Miss
Utalii Tanzania, tunapata udhamini wa mamlaka za utalii, wakati ukweli ni
kwamba hakuna udhamini kama huo. Licha ya ukweli kuwa katika umri wake wa miaka
Miss Utalii Tanzania ndilo shindano lenye mafanikio makubwa zaidi kitaifa na
kimataifa kuliko mashindano mengine yoyote nchini na hata Afrika mashariki na
kati. Udhamini ni changamoto na kikwazo kikuu cha kufikia 100% ya malengo ya
shindano letu na hata ndoto yetu ya kulifanya kuwa shindano bora zaidi nchini,Afrika
na hata Duniani. Baadhi ya mataji ya Dunia tunayo shikilia ni pamoja na Miss
Tourism World 20050 - Africa, Tourism Model Of The World 2006- Personality,
Miss Tourism World 2006- SADC, Miss Africa 2006 – 1st Runner Up,
Miss Tourism World 2007- Africa, Miss Freedom Of The World 2013, Miss Tourism
World 2008 -Internet, Miss United Nation 2009.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT MIKUMI NATIONAL PARK |
Miss Utalii Tanzania ni shindano la kwanza nchini kutwaa taji la Dunia kabla na
baada ya uhuru na kuipa Tanzania heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za Dunia
2006. Rais wa Miss Tourism Tanzania Organisation Gideon Chipungahelo, ni mtanzania
wa kwanza kuteuliwa katika uongozi wa ngazi ya Dunia wa Urembo, ikiwemo
nyadhifa za Mkurugenzi Bara la Afrika Miss Tourism World Organisation, Miss
United Nation Organisation na Makamu wa Rais Dunia World Beauty Pageant
Association, Miss Tourism University World Organisation na Miss Heritage World
Organisation. Ili kukabiliana na changamoto hizi, bodi ya mashindano imebadili
sera na mfumo wa uongozi na uendeshaji mashindano, kutoka katika mfumo wa kuwa
shindano la kibiashara hadi kuwa shindano la kijamii (Non Profit Making),
kutoka katika mfumo wa kufanya shindano stejini kuanzia ngazi za chini hadi
katika mfumo wa kufanya mashindano stejini kuanzaia katika ngazi za kanda na
klanda maalum za vyuo vikuu, kutoka katika mfumo wa kuwa na kamati na mawakala
hadi katika mfumo wa kuwa na wakurugenzi waajiliwa wa ngazi za kanda hadi taifa,
na kuwa na kamati zenye majina makubwa hadi kamati za wataalam watendaji.
MISS TOURISM TANZANIA 2013 AT MIKUMI NATIONAL PARK
Kutoka katika mfumo wa onyesho la viingilio hadi katika mfumo wa onyesho lisilo
na viingilio, kutoka katika mfumo wa onyesho la ukumbini hadi katika mfumo wa
onyesho la TV Show. Kutoka katika mfumo wa kuweka kambi katika mahoteli hadi
katika mfumo wa kuweka kambi katika Miss Tourism Houses na Tourist Attractions
Camp Sites, kutoka katika mfumo wa kuwa shindano la kitaifa hadi katika mfumo
wa kuwa shindano la kimataifa, lenye washiriki kutoka mabara yote duniani.
Kwa
mfumo huu mpya, washindi wa ngazi za majimbo,wilaya na mikoa watapatikana kwa
njia ya Odiashion. Kwa mfumo huu mpya kila mbunge atakuwa na mrembo wake wa
Utalii, Kila Mkuu wa Wilaya atakuwa na Mrembo wake wa Utalii na Kila Mkuu wa
Mkoa atakuwa na Mrembo wake wa Utalii. Lakini pia mfumo huu utadhibiti hujuma
na ,umamluki, udanganyifu wa sifa za washiriki lakini pia kuondoa tatizo la
warembo wasio na sifa , wasio natabia njema na mwenendo mwema katika jamii. Kwa
mfumo huu wa TV Show, fainali zote kuanzia ngazi ya kanda zitarushwa LIVE
katika TV na mitandao ya Internet. Aidha kwa mfumo huu tutakuwa na kituo chetu
cha Televisheni cha Miss Tourism (Miss UTalii TV).
MISS TOURISM TANZANIA 2013 |
Mkakati
huu, ni mkubwa na unahitaji muda na umakini wa hali ya juu, pia wataalam wa
ndani na nje kuufanikisha . Hivyo bodi imeona ni vyema kujipa muda wa mwaka
(Msimu) mmoja kujipanga bila ya kufanya mashindano. Hapa ieleweke kuwa hatuja
simamisha shughuli za kampuni za kutangaza na kuhamasisha utalii na utamaduni,
bali tumesimamisha shindano la msimu wa 2013/2014, huku washindi wa msimu wa
2012/2013 wakiendelea na majukumu yao kama kawaida , ikiwemo kuwakilisha Taifa
katika mashindano ya Dunia na kimataifa 2013/2014 kama ifuatavyo na nchi yanakofanyika
katika mabano ni,
THE MISS TOURISM TANZANIA 2013 |
Miss
Tourism World 2013 ( Equatorial Guinea), Miss Face Of The World 2013 ( Afrika
Kusini) , Miss Heritage World 2013 (China) Miss Tourism United Nation 2013 (
Marekani), Miss International 2013 ( Japani), Miss Planet 2013 ( Ufaransa ),
Miss Tourism University World 2013 (Uingereza).
MISS TOURISM TANZANIA 2013 |
Aidha
bodi imetoa onyo kali kwa yeyote atakaye thubutu au kujaribu tena kuhujumu
shiondano hili kwa namna yoyote, kwani atakumbana na hatua kali za kisheria
bila ya kujali wadhifa, mamlaka, jinsia au rangi. Bodi pia imewataka maadui na
mamluki wote kujiondoa katika shindano hili na ngazi mbalimbali za uongozi na
mataji kabla ya kuondolewa, kwani mchakato ujao hautalengwa kwa jiwe.
Erasto
Gideon Chipungahelo
Mwenyekiti
Mtendaji
Miss
Tourism Tanzania Organisation (MTTO)
No comments:
Post a Comment