Liverpool walipelekwa Dakika 120 kwenye Mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Ligi, CAPITAL
ONE CUP, walipocheza na Timu iliyo Daraja la 3, Ligi 1, Notts County na
kutoka Sare 2-2 katika Dakika 90 na hatimae kushinda 4-2 kwenye Dakika
za Nyongeza 30 na kutinga Raundi ya Tatu.
Liverpool waliongoza 2-0 kwa Bao za
Raheem Sterling na Daniel Sturridge lakini Kipindi cha Pili Yoann Arquin
na Adam Coombes wakaisawazishia Notts County na Mechi kwisha 2-2 katika
Dakika 90.
Katika Dakika za Nyongeza 30, Sturridhe na Jordan Henderson wakaipa Liverpool Bao 2 na kushinda 4-2.
Timu nyingine za Ligi Kuu England ambazo
zilishinda Jana ni WBA, Sunderland, Southampton, Fulham [kwa Penati],
Norwich, Hull City na West Ham.
Crystal Palace ilibwagwa 2-1 na Bristol City.
Katika Raundi ya Tatu, zile Timu za Ligi
Kuu England ambazo zinashiriki Mashindano ya UEFA Ulaya, UEFA CHAMPIONZ
LIGI na EUROPA LIGI, zitaanza kushiriki.
Raheem Sterling ndiye aliyeifungulia bao la kwanza Liverpool
Sterling akiuvuta mpira
Aly Cissokho aliumia na kulazimika kutolewa nje
Kolo Toure hakujiweza ..alibebwa na stretcher na kutolewa nje ...
Kapteni wa Gerard Liverpool akionesha alama ya vidole ya 2-2 kwa maana ngoma bado mbichi
mchezaji Joss Labadie wa Notts County kwenye patashika kugombea mpira jana usiku
Yoann Arquin akitupia kwa kichwa na mpira kugonga posti
Adam Coombes akishangilia baada ya kusawazisha
Coombes (No 14) akipongezwa na wenzake na mpira kusonga mbele kwa dakika 120
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet, Johnson,
Toure, Wisdom, Cissokho (Agger 10min), Gerrard, Allen (Henderson 65),
Alberto (Countinho 72), Ibe, Sturridge, Sterling. Subs not used: Brad Jones, Aspas, Lucas, Borini.
Booked: Wisdom, Sterling.
Goals: Sterling 4, Sturridge 29, 105, Henderson 110.
Notts County: Bialkowski, Dumbuya, Liddle, Smith, Stevens, Bell (Coombes 82), Labadie, Fotheringham (Boucaud 72), Campbell-Ryce (Thompson 71), Arquin, McGregor.
Subs not used: Murray, Spiess, Tempest, Nangle.
Booked: Campbell-Ryce, Arquin
Goals: Arquin 62, Coombes 84.
Attendance: 42,231.
No comments:
Post a Comment