Chelsea imekubali kulipa pauni millioni 30 kumsajiliwa kiungo mchezaji Willian kutoka klabu ya Urussi Anzhi Makhachkala.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Brazilia alikaribia kusaini mkataba na Tottenham baada ya vipimo vya afya siku ya jumaatano.
Lakini inafahamika kuwa Chelsea walijitosa mnamo siku ya Alhamisi na kupendekeza kitita hicho na kukubaliana na mchezaji huyo.
Mkataba huo umewezekana baada ya kuingilia kati kwa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich, ambaye bepari mwenzake Mrussi Suleyman Kerimov anamiliki klabu ya Anzhi
Willian alitazamia kujiunga na Tottenham, lakini Chelsea ilipojitoa aliamua asikose fursa ya kucheza kwenye kombe la klabu bingwa ya Ulaya.
Kwa mujibu wa duru za klabu hiyo Chelsea imekua ikimrandia mchezaji huyo tangu 2011.
Willian ni mchezaji wa tatu kusajiliwa Stamford Bridge baada ya Mjerumani Andre Schurrle na Marco van Ginkel wa Uholanzi.Kitendo hicho cha Spurs kumkosa Willium wenda kikamchelewesha Bale kwenda Real Madrid wiki hii...

No comments:
Post a Comment