BUKOBA SPORTS

Friday, August 30, 2013

DIAMOND AMKABIDHI GARI MZEE GURUMO WAKATI WA KUTAMBULISHA VIDEO YAKE YA MY NUMBER ONE

Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo kama zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi kuimba muziki, Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla yake ya uzinduzi wa video yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi huko Afrika Kusini ikigharimu kiasi cha dola elfu 30.000 zaidi ya milioni arobaini za Tanzania, Video hiyo imetengenezwa kwa viwango vya kimataifa na itaweza kumtangaza vyema kijana huyo wa kitanzania katika ulimwengu wa muziki hasa kimataifa, Hafla hiyo imefanyika kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam na imehudhuriwa na wasanii pamoja na waigizaji wa filamu na watu maarufu mbalimbali Mzee Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari Akimuelekeza jambo baada ya mzee Gurumo kuingia kwenye gari
MSANII Nassib Abdulmalick maarufu kama Diamond Platinum, ameonyesha yeye ni mkali na mwenye fedha nyingi baada ya kukusanya watu kibao katika hoteli ya Serena, Posta, jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa video yake ya My Number One.


Msanii Diamond akiwa Serena Hoteli alipozindua video ya wimbo wake wa My Number One.
Mbali na uzinduzi huo, pia msanii alitumia fursa hiyo kumkabidhi gari alilomnunulia mwanamuziki mkongwe nchini, Muhidin Gurumo, aliyestaafu muziki, huku akisema hajafanikiwa kununua hata baiskeli.


Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo kama zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi kuimba muziki, Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla yake ya uzinduzi wa video yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi huko Afrika Kusini

Mzee Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo

Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari

Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari

Akimuelekeza jambo baada ya mzee Gurumo kuingia kwenye gari

Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari

Mzee Ngurumo amesema"Haamini macho na masikio yake,hanachakusema zaidi ya ASANTE kwa msanii huyo"Lakini pia amesema hajui hata mke wake atasemaje baada ya kumwona akiingia na gari ndani ya nyumba yake. Mzee ngurumo amekuwa na matatizo ya kiafya siku za karibuni nakupelea kustaafu mziki kabisa.Wazee wa msondongoma ndio wanajua makali ya Mzee Ngurumo.


Picha ya pamoja Ney wamitego, Madam Rita pamoja na Diamond

Katika mazungumzo yake, Diamond alisema kuwa anathamini mchango wa wanamuziki waliyotangulia, kwakuwa wao ndio waliyosababisha sanaa yao izidi kuchanja mbuga.
"Namthamini mno mzee Gurumo na wanamuziki wengine wote wa Tanzania, maana bila wao sisi tusingeweza kusimama hapa tulipokuwa sasa, ukizingatia kuwa wao ndio kila kitu," alisema Diamond.

Naye mzee Gurumo alisema haamini macho yake baada ya kupewa ufunguo wa gari lililonunuliwa na msanii Diamond, ambaye kwake ndio chaguo kwa waimbaji wa Bongo Fleva,.

"Namshukuru huyu kijana na Mungu ampe mafanikio makubwa zaidi katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya ili aendelee kuwa juu zaidi kwa kitendo chake hiki ambacho kinashangaza wengi," alisema.

Diamond ndio msanii wa kwanza kufanya kitendo cha kiungwana kama hicho, huku pia mkutano wake ukifana kwa kualika wadau mbalimbali wenye majina yao kwa ajili ya kushuhudia anachofanya ndani ya Hoteli ya Nyota tano ya Serena, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment