Droo ya ligi ya soka ya Europa barani Ulaya imetolewa siku ya Ijumaa na vlabu kugawanywa katika makundi 12.
Klabu ya Swansea ya Uingereza itamenyana na Valencia ya Uhispania katika kundi la A huku Tottenham Hotspur pia ya Uingereza ikipangwa katika kundi moja na Anzhi Makhachkala ya Urusi.
Wachambuzi wa soka wanasema kuwa Swansea itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Valencia, huku Tottenham Hotspurs wakionekana kupata timu nyepesi na hivyo wanatarajiwa kufuzu kwa urahisi.
Hivi ndivyo vilabu mbalimbali vilivyopangwa katika ligi kuu ya Europa.
Kundi A: Valencia, Swansea, Kuban, St Gallen
Kundi B: PSV Eindhoven, Dinamo Zagreb, Chornomorets Odesa, Ludogorets
Kundi C: Standard Liège, Salzburg, Elfsborg, Esbjerg
Kundi D: Rubin, Wigan Athletic, Maribor, Zulte Waregem
Kundi E: Fiorentina, Dnipro, Paços Ferreira, Pandurii
Kundi F: Bordeaux, APOEL, Eintracht Frankfurt, Maccabi Tel Aviv
Kundi G: Dynamo Kyiv, Genk, Rapid Wien, Thun
Kundi H: Sevilla, Freiburg, Estoril, Liberec
Kundi I: Lyon, Betis, Guimarães, Rijeka
Kundi J: Lazio, Trabzonspor, Legia, Apollon
Kundi K: Tottenham, Anzhi Makhachkala, Sheriff, Tromsø
Kundi L: AZ Alkmaar, PAOK, Maccabi Haifa, Shakhter Karagandy
No comments:
Post a Comment