Monday, August 26, 2013

MANCHESTER CITY WALA KICHAPO CHA KWANZA MBELE YA KOCHA WAO MPYA NA PELLEGRINI LIGI KUU ENGLAND MSIMU 2013/2014

Hiki ni kichapo cha kwanza kwa Man City kumkaribisha meneja mpya wa Manuel Pellegrini katika ligi ya England.
Mabao mawili yaliyotiwa kimiani na mshambuliaji Fraizer Campbell yameipa ushindi Cardiff City wa magoli 3-2 dhidi ya Manchester City leo kwenye uwanja wa Cardiff.

Edin Dzeko alikuwa ametangulia kuifungia bao City kunako dakika ya 52 lakini likasawazishwa baadae na Aron Gunnarsson. Kona mbili zilitosha kuiangamiza jana City muuaji wa bao hizo akiwa na mchezaji wa zamani wa Manchester United Campbell.
*Leo usiku Saa 4:00 usiku Manchester United wataikaribisha Chelsea kwenye uwanja wao wa Old Trafford.

No comments:

Post a Comment