Monday, August 26, 2013

PICHA: DILLISH KUTOKA NAMIBIA NDIYE MSHINDI WA BBA THE CHASE


Mshindi wa Big Brother The Chase 2013, Dillish Matthews.
MWANADADA Dillish Matthews kutoka nchini Namibia amejishindia zaidi ya shilingi milioni 480 (300,000 usd) baada ya kuibuka mshindi wa Big Brother The Chase 2013.Dillish amewabwaga washiriki wenzake wanne Beverly, Melvin, Cleo na Elikem alioingia nao tano bora. Wa kwanza kutolewa tano bora alikuwa Beverly akifuatiwa na Melvin baadaye akafuata Elikem na kuwaacha Dillish na Cleo wakichuana kutafuta mshindi wa dola 300,000 za Kimarekani. Hatimaye Cleo naye aliondolewa katika kinyang'anyiro hicho na kumuacha Mnamibia Dillish na hatimaye kutwaa kitita hicho kikubwa cha fedha.

NCHI ZILIZOMPIGIA KURA DILLISH NA NI KAMA HIVI:
Angola: Dillish
Botswana: Cleo
Ghana: Elikem
Kenya: Dillish
Ethiopia: Beverly
Malawi: Cleo
Namibia: Dillish
Nigeria: Melvin
South Africa: Cleo
Sierra Leone: Elikem
Tanzania: Dillish
Uganda: Dillish
Zambia: Cleo
Zimbabwe: Elikem
Rest of Africa: Melvin
Total: Dillish = 5, Cleo = 4, Elikem = 3, Melvin = 2, Beverly = 1.

No comments:

Post a Comment