Lakini Ancelotti, Kocha wa Real Madrid, amesema Nyota hao ambao ndio Wachezaji wa Bei ghali Duniani wanaweza kucheza Timu moja na yeye sasa anatafakari mfumo murua wa kuweza kwao kuwa pamoja bila ya kumbadilisha na kumweka Ronaldo kama Sentafowadi.
Ancelotti amesisitiza: “Hapana, Ronaldo hawezi kuwa Sentafowadi, sasa tunatayarisha fomesheni ya kuwawezesha wote wawili kwa pamoja waonyeshe ubora wao. Lazima uwaweke Wachezaji bora kwenye nafasi ambazo wanajisikia vyema. Kila kitu kinakwenda sawa. Real Madrid ni Klabu kubwa na imejipanga vyema.”
Ancelotti ameshika wadhifa hapo Real Madrid mwanzoni mwa Msimu huu baada ya kuondoka kwa Jose Mourinho ambae amehamia Chelsea na mwenyewe amesisitiza hana presha kwenye kazi yake mpya.
Amesema: “Ni kitu cha kawaida kwa Kocha. Kote kuna presha kubwa hapa Real Madrid na hata kule nlikotoka Paris Saint-Germain. Kila Timu ipo presha ya kufikia malengo yake. Baada ya Miaka mingi ya uzoefu unazoea hii presha!”
Hadi sasa kwenye La Liga, Real Madrid imecheza Mechi 3 na kushinda zote na imefungana na Barcelona, Atletico Madrid na Vilareal ambazo nazo zimeshinda Mechi zao zote tatu.
RATIBA
Jumamosi Septemba 14
17:00 Atletico de Madrid v UD Almeria
19:00 Levante v Real Sociedad
21:00 FC Barcelona v Sevilla FC
23:00 Villarreal CF v Real Madrid CF
Jumapili Septemba 15
13:00 Granada CF v RCD Espanyol
18:00 Getafe CF v Osasuna
20:00 Malaga CF v Rayo Vallecano
22:00 Real Betis v Valencia
Jumatatu Septemba 16
21:00 Elche CF v Real Valladolid
23:00 Athletic de Bilbao v Celta de Vigo
Ijumaa Septemba 20
22:00 Osasuna v Elche CF
No comments:
Post a Comment