ARSENAL KUKWAANA NA CHELSEA KOMBE LA LIGI, CAPITAL ONE CUP
KLABU ya Arsenal imepangwa kuchezwa na Chelsea katika mchezo wa Kombe la Ligi mzunguko wa nne kwenye ratiba ya michuano hiyo iliyopangwa jana. Arsenal ilitinga hatua hiyo baada ya kuifunga West Bromwich Albion kwa changamoto ya mikwaju ya penati wakati Chelsea wao walisonga mbele kwa ushindi dhidi ya timu ya daraja la pili ya Swindon Town. Theo Walcott akishangilia moja ya bao la ushindi alioupatia ArsenalKwa upande mwingine Manchester United ambao wamewang’oa mahasimu wao Liverpool jana wamepangiwa kucheza na Norwich City katika Uwanja wa Old Traford. Timu zingine ni Tottenham Hotspurs watakwaana na Hull City, Newcastle United watacheza na Manchester City huku Sunderland wakiikaribisha Southampton. Mechi za mzunguko wa nne zinatarajiwa kuchezwa wiki inayoanzia Octoba 28 mwaka huu.
RATIBA KAMILI RAUNDI YA NNE CAPITAL ONE
Sunderland v Southampton Leicester City v Fulham Birmingham City v Stoke City Manchester United v Norwich City Burnley v West Ham United Arsenal v Chelsea Tottenham v Hull City Newcastle v Manchester City
No comments:
Post a Comment