BUKOBA SPORTS

Thursday, September 12, 2013

ARSENE WENGER AKUMBWA NA UHABA WA WASHAMBULIAJI, ABAKI NA GIROUD PEKEE!! PODOLSKI, SANOGO, BENDTNER, CHU-YOUNG MAJANGA!!


Kocha Arsene Wenger, anakabiliwa na upungufu wa Masentafowadi baada ya Yaya Sanogo kuungana na Lukas Podolski kwenye Listi ya Majeruhi na hivyo kubakiwa na Straika mmoja tu, Olivier Giroud, kwenye Kikosi chake ambacho Jumamosi kitacheza Mechi ya Ligi Kuu England huko Stadium of Light dhidi ya Sunderland.
Yaya Sanogo alipata maumivu yake wakati akiwa na Timu ya Taifa ya France U-21 hivi Juzi na mapema kurudishwa Klabuni kwake Arsenal kwa matibabu.
Lukas Podolski yeye amethibitishwa atakuwa nje kwa Miezi mitatu akitibiwa Musuli za Pajani.
Mbali ya Giroud, Wenger anaweza kumtumia Theo Walcott kama Sentafowadi ingawa Meneja huyo hupendelea kumchezesha kwenye Winga ya kulia.

Lakini Arsenal wanae Straika wao wa zamani kutoka Denmark, Nicklas Bendtner, ambae kwa kipindi alikuwa nje kwa Mkopo lakini amerudi tena huko Emirates ingawa inasemekana hayuko fiti kwa ajili ya Mechi.

Pia Arsenal wanae Fowadi wa South Korea, Park Chu-Young, ambae Jina lake limo kwenye Kikosi cha Wachezaji 25 kilichosajiliwa kwa ajili ya Ligi Kuu England lakini nae pia inadaiwa hayuko fiti kwa Mechi.

Katika Kipindi cha Uhamisho kilichofungwa Septemba 2, Arsenal ilihusishwa na kuwasaini Mastraika hatari kina Luis Suarez, Gonzalo Higuain, Wayne Rooney, Karim Benzema na Demba Ba lakini mwishowe hawakumpata hata mmoja.

No comments:

Post a Comment