BUKOBA SPORTS

Thursday, September 12, 2013

ATHUMAN CHIUNDI ATWAA KOMBE LA GOFU LA CDF LUGALO




Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima



Egino Chusi akicheza gofu kwenye fainali za Lugalo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima akimkabdi Abdallah Yusuph

Bingwa wa Kombe la CDF yaliyoandaliwa na klabu ya Lugalo na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi. akiwa ameshika kombe la Mkuu wa Majeshi na kombe alilokabidhiwa. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima,

MCHEZAJI Athuman Chiundu ameibuka bingwa wa mashindano ya gofu ya kombe la CDF yaliyoandaliwa na klabu ya Lugalo na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi.
Abdala katika siku ya kwanza alipiga gofu 71 na siku ya pili alipiga 70 na kumaliza akiwa amefikisha 141 na kumfanya kuwa bingwa na kuzawadiwa kikombe pamoja na jokofu dogo.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Abdallah Yusuph ambaye alipiga gofu 151 na kupata kombe na pamoja na macrowaves.

Kwa upande wa wanawake Vicky Elias alishika nafasi ya pili na kufanikiwa kupata kombe na rice cooker huku nafasi ya kwanza ikienda kwa Hitech Valambia.

Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima, alisema anashukuru kwa udhamnini wa kinywaji cha konyagi kwani imepanua wigo wa wachezaji kuongezeka.

“Nashukuru Konyagi kwa udhamini wao kwani umesaidia kuongeza idadi ya washiriki hadi kufikia 72 kwa mwaka huu”, alisema Masima
Mashindano hayo ambayo ni mara ya nne yakichezwa yalianza kutimua vumbi Septemba 7 na kumalizika Septemba 8 na yalishirikisha wachezaji maarufu kama Gidioni Sayore, GM Waitara, na Victor Kimesera

No comments:

Post a Comment